FACEBOOK INC. NA THE EU-U.S. na SWISS-U.S. NGAO YA FARAGHA
Facebook Inc. (“Facebook”) imeidhinishwa kwenye EU-U.S. Mfumo wa Ngao ya Faragha na Swiss-U.S. Mfumo wa Ngao ya Faragha (kwa pamoja, “Mifumo ya Ngao ya Faragha”) na U.S. Idara ya Biashara inayohusiana na mkusanyiko na uchakataji wa data ya kibinafsi kutoka kwa watangazaji, wateja, au washirika wetu wa biashara katika Muungano wa Ulaya na, mahali ambapo mdhibiti data wa Uswisi hutumia Facebook kama kichakataji cha data, Uswisi (“Washirika”) kuhusiana na bidhaa na huduma zilizofafanuliwa kwenye sehemu ya Upeo hapa chini na kwenye uhalalishaji wetu. Ili kujifunza zaidi kuhusu programu ya Ngao ya Faragha tafadhali tembelea www.privacyshield.gov.
Upeo: Facebook inazingatia Kanuni za Ngao ya Faragha (kama ilivyowekwa katika kila Mifumo ya Ngao ya Faragha) kwa maeneo yafuatayo ya biashara yetu (kwa pamoja “Huduma za Mshirika”):
  • Workplace ya Facebook: Workplace ni huduma ambayo huruhusu watu kushirikiana kwa ufanisi zaidi na kushiriki maelezo kazini. Washirika (waajiri au mashirika - wadhibiti wa data) wanaweza kuwasilisha maelezo ya kibinafsi kuhusu wanachama kwenye Facebook, pamoja na Facebook Ireland kama kichakataji na Facebook Inc. kama kichakataji kidogo. Wakati Washirika na wanachama wao wanaamua maelezo ya kuwasilisha, kwa kawaida yanajumuisha mambo kama maelezo ya waasiliani wa biashara, wateja na wafanyikazi, maudhui yaliyozalishwa na mfanyikazi na mawasiliano, na maelezo mengine chini ya udhibiti wa Mshirika. Kwa maelezo zaidi, wanachama wanaweza kuwasiliana na Mshirika ambaye wana akaunti ya Workplace naye na kukagua sera ya faraghaya Workplace.
  • Matangazo na Vipimo: Facebook inatoa bidhaa za Matangazo na Vipimo na kupitia kwa huduma hizo Facebook inaweza kupokea data kutoka kwa Washirika wasio na uhusiano (wadhibiti wa data) ambapo Facebook Ireland ni kichakataji na Facebook Inc. ni kichakataji kidogo. Hii hujumuisha mambo kama maelezo ya mwasiliani na maelezo kuhusu hali wanayopitia watu binafsi au miingiliano na Washirika na bidhaa, huduma na matangazo yao. Kwa maelezo zaidi kuhusu bidhaa za matangazo na vipimo, tembelea ukurasa wetu wa Kuhusu Utangazaji kwenye Facebook na Sera yetu ya Data.
Facebook hutumia data ya binafsi iliyotolewa na Washirika wetu ili kutoa Huduma za Mshirika kulingana na sheria zinazotumia kwa Huduma muhimu za Mshirika na vinginevyo maagizo ya Washirika. Facebook hufanya kazi pamoja na Washirika wake ili kuhakikisha kuwa watu binafsi wamepewa chaguo sahihi zinazotumika chini ya Kanuni za Ngao ya Faragha.
Ufikiaji. Ndani ya upeo wa uidhinishaji wwtu kufanya hivyo, na kulingana na juhudi zetu chini ya Ngao ya Faragha, Facebook itafanya kazi na Washirika wake kutoa idhini ya ufikiaji kwa watu binafsi hadi data ya binafsi kuwahusu ambayo Facebook iko nayo kwa niaba ya Washirika wake. Facebook pia huchukua hatua zinazofaa ili kuwezesha watu binafsi, moja kwa moja au kwa muunganisho na Washirika, kusahihisha, kurekebisha, au kufuta data ya binafsi ambayo imeonyeshwa kutokuwa sahihi.
Washirika Wengine. Facebook inaweza kuhamisha data ndani ya Familia ya kampuni za Facebook na mashirika mengine, yakijumisha watoa huduma na washirika wengine. Kulingana na Kanuni za Ngao ya Faragha, Facebook inawajibikia uchakataji wowote wa data ya binafsi na wahusika wengine ambao hawaambatani na Kanuni za Ngao ya Faragha isipokuwa endapo Facebook haikuwajibikia tukio lililosababisha uharibifu unaodaiwa.
Maombi ya Kisheria. Data ya kibinafsi tunayohamishiwa na Washiriki wetu inaweza kufichuliwa kulingana na maombi ya kisheria au mchakato mwingine wa mahakama au serikali, kama vile ilani, dhamana, au maagizo. Kwa maelezo zaidi, kagua sehemu ya “Je, tutajibu vipi maombi ya kisheria au kuzuia uharibifu?” ya Faragha ya Data ya Facebook na sehemu ya “Maombi ya Kisheria” ya Sera ya Faragha ya Workplace.
Utekelezaji. Uzingatiaji wa Facebook kwa Kanuni za Ngao ya Faragha unazingatia mamlaka ya uchunguzi na utekelezaji ya Marekani. Tume ya Biashara ya Shirikisho.
Maswali na Migogoro. Tafadhali wasiliana nasi kwa maswali na malalamishi yoyote yanayohusu uhalalishaji wetu wa Ngao ya Faragha. Una chaguo la kutatua migogoro yoyote uliyo nayo nasi kulingana na uhalalishaji wetu kupitia TRUSTe, mtoaji wa utatuzi mbadala wa mgogoro nchini Marekani. Unaweza kuwasiliana na TrustArc kupitia tovuti yao. Katika hali nyingine, Mfumo wa Ngao ya Faragha hutoa haki ya kubatilisha usuluhishi unaopatanisha ili kutatua malalamishi ambayo hayajatatuliwa kwa njia nyingine, kama ilivyofafanuliwa katika Annex I kwenye Mifumo ya Ngao ya Faragha. Kwa kuongezea, kama sehemu ya Mifumo ya Ngao ya Faragha, Marekani Idara ya Mratibu Mkuu ya Taifa inachukua nafasi ya Ombudsperson ili kuwezesha uchakataji wa maombi yanayohusiana na ufikiaji wa usalama wa taifa kwa data inayohamishwa kutoka Muungano wa Ulaya na Uswisi (kwa mtiririko huo) hadi Marekani.
Kwa maelezo zaidi kuhusu maadili ya faragha ya Facebook tafadhali kagua Sera yetu ya Faragha.