Masharti ya Huduma ya Workplace


UNADHAMINI NA KUWAKILISHA KWAMBA UNAINGIA KATIKA MASHARTI HAYA YA MTANDAONI YA WORKPLACE (“MAKUBALIANO”) KWA NIABA YA KAMPUNI AU SHIRIKA LINGINE LA KISHERIA NA KWAMBA UNA MAMLAKA KAMILI YA KUHUSISHA SHIRIKA KAMA HILO KATIKA MAKUBALIANO HAYA. KUREJELEWA KWA “WEWE”, “YAKO” AU “MTEJA” KUNA MAANA YA SHIRIKA KAMA HILO.
Ikiwa eneo lako msingi la biashara lipo Marekani au Kanada, Makubaliano haya ni makubaliano kati yako na Meta Platforms, Inc. Vinginevyo, Makubaliano haya ni makubaliano kati yako na kampuni ya Meta Platforms Ireland Ltd. Kurejelewa kwa “Meta”, “nasi”, “sisi”, au “yetu” kuna maana ya Meta Platforms, Inc. au Meta Platforms Ireland Ltd., kama inavyofaa.
Masharti yafuatayo yatatumikwa kwa matumizi yako ya Workplace. Unakiri kwamba vipengele na utendaji wa Workplace unaweza kutofautiana na unaweza kubadilika kwa muda.
Istilahi fulani zilizoendelezwa kwa herufi kubwa zimefafanuliwa katika Sehemu ya 12 {Ufafanuzi} na nyingine zimefafanuliwa katika muktadha kwenye Makubaliano haya.
  1. Matumizi ya Workplace
    1. Haki Zako za Utumiaji. Katika kipindi cha Masharti haya, una haki isiyobagua, isiyoweza kuhamishwa, isiyoweza kutolewa leseni kwa watu wengine ya kufikia na kutumia Workplace kwa mujibu wa Makubaliano haya. Matumizi ya Workplace hupatikana tu kwa Watumiaji (wakiwemo, panapotumika, wale wa Washirika wako) ambao umewawezeshea akaunti na unawajibikia Watumiaji wote na uzingatifu wao wa Makubaliano haya na kufikia na kutumia kwao Workplace. Ili uwazi, Workplace inatolewa kama huduma kwako wala sio kwa Watumiaji kibinafsi.
    2. Akaunti. Maelezo yako ya usajili na ya akaunti ya msimamizi lazima yawe sahihi, kamilifu na yamesasishwa. Akaunti za watumiaji ni za Watumiaji binafsi na haziwezi kushirikiwa wala kuhamishwa. Lazima uweke maelezo ya kuingia kwenye akaunti kwa siri na ukubali kuarifu Meta mara moja ikiwa utagundua matumizi yoyote maelezo yako ya akaunti au ya kuingia kwenye akaunti.
    3. Vikwazo. Hutatumia (na hutaweza kumpa mtu yeyote mwingine leseni): (a) kutumia Workplace kwa niaba ya mshirika mwingine au kukodisha, kukodisha kwa muda, kutoa uwezo wa kufikia au kutoa leseni ya kutumia Workplace kwa washirika wengine, isipokuwa Watumiaji walioruhusiwa hapa ndani ; (b) kubadilisha uhandisi, kutenganisha data, kugawa, au vinginevyo kutaka kupata msimbo wa chanzo wa Workplace, isipokuwa kadri ilivyoruhusiwa moja kwa moja na sheria tumika (kisha baada ya notisi ya mapema kwa Meta); (c) kunakili, kukarabati au kuunda kazi zalishwa za Workplace; (d) kuondoa, kukarabati au kuficha notisi zozote za haki miliki au notisi nyingine zilizo kwenye Workplace; au (e) kusambaza maelezo ya kiufundi kuhusu utendakazi wa Workplace.
    4. Usanidi. Wakati wa kusanidi toleo lako la Workplace, utatua Mtumiaji mmoja au zaidi kama msimamizi au wasimamizi wa jumuiya yako ya Workplace ambaye anawajibikia usimamizi wa toleo lako la Workplace. Lazima uhakikishe kwamba una angalau msimamizi mmoja wa mfumo kwa ajili ya toleo lako la Workplace kila wakati.
    5. API ya Workplace. Katika kipindi cha kutumika kwa Masharti, Meta inaweza kukutolea API moja au zaidi ya Workplace, ili uweze kuunda na kutumia huduma na programu ambazo zinatumika pamoja na Workplace. Matumizi yoyote ya API ya Workplace na wewe, Watumiaji wako au mhusika yeyote mwingine kwa niaba yako kutatawaliwa na masharti ya sera ya Jukwaa la Workplace (inayopatikana hapa kwa sasa: workplace.com/legal/WorkplacePlatformPolicy, na kama ilivyobadilishwa na Meta kila mara).
    6. Msaada. Tunatoa msaada wa Workplace kwako kupitia kichupo cha moja kwa moja cha usaidizi kilicho kwenye paneli ya msimamizi wa Workplace (“Kituo cha Msaada wa Moja kwa Moja”). Unaweza kuwasilisha ombi la msaada ili kutatua swali fulani, au kuripoti tatizo, kuhusiana na Workplace, kwa kufungua tikiti kwenye Kituo cha Msaada wa Moja kwa Moja (“Tikiti ya Msaada”). Tunatoa mwitikio wa awali kwa kila Tikiti ya Msaada ndani ya saa 24 kutoka wakati umepokea barua pepe ya kuthibitisha kwamba Tikiti yako ya Msaada imefunguliwa halali kupitia Kituo cha Msaada wa Moja kwa Moja.
  2. Data na Wajibu Wako
    1. Data Yako. Chini ya Makubaliano haya:
      1. Unasalia na haki zote, hati na mapendeleo (zikiwemo haki za mali ya akili) katika na kwa Data yako;
      2. Masharti yanapotumika, unaipa Meta haki isiyobagua, ya ulimwengu kote, isiyo na riba, na iliyolipiwa kikamilifu ya kutumia Data Yako kwa madhumuni pekee ya kukutolea Workplace (na usaidizi unaohusiana) kwa mujibu wa Makubaliano haya; na
      3. Unakiri kwamba Meta ndiyo mchakataji data na kwamba wewe ndiwe mdhibiti data wa Data Yako na kwa kuingia katika Makubaliano haya, unaelekeza Meta kuchakata Data Yako kwa niaba yako, kwa malengo yaliyobainishwa katika Makubaliano haya pekee na kwa mujibu wa Makubaliano haya (kikiwemo Kiambatisho cha Uchakataji Data).
    2. Wajibu Wako. Unakubali (a) kwamba unawajibu kipekee wa kuhakikisha Data Yako na maudhui yake ni sahihi; (b) kutafuta haki zote na vibali vyote muhimu vinavyohitajika Kisheria kutoka kwa Watumiaji wako na mhusika yeyote mwingine tumika ili kuruhusu ukusanyaji na matumizi ya Data Yako yalivyoelezwa katika Makubaliano haya; na (c) kwamba matumizi yako ya Workplace, ikiwemo Data Yako na matumizi yake hapa, hayatakiuka Sheria zozote au haki za wahusika wengine, zikiwemo haki za mali ya akili, ufaragha na matangazo. Ikiwa Data Yako yoyote itatumwa au kutumiwa kwa kukiuka Sehemu hii ya 2, unakubali kuiondoa haraka kutoka kwenye Workplace. Unawajibikia uamuzi wowote wa kushiriki Data Yako miongoni mwa Watumiaji au na wahusika wengine, na Meta haiwajibikii matumizi, ufikiaji, urekebishaji, usambazaji au kufutwa kwa Data Yako na wale watu ambao wewe au Watumiaji wako wamewafanya kupatikana.
    3. Data iliyopigwa Marufuku. Unakubali kutowasilisha kwa Workplace, maelezo yoyote au data ambazo zinahusu kulinda na/au vikwazo dhidi ya usambazaji kwa mujibu wa sheria na/au kanuni tumika (“Maelezo Yaliyopigwa Marufuku”). Kuhusu maelezo ya kiafya, unakiri kwamba Meta si Mshirika wa Kibiashara au mwanakandarasi mwingine (kwa vile maneno hayo yamefafanuliwa katika Sheria ya Bima ya Afya na Uwajibikaji (“HIPAA”)) na kwamba Workplace haizingatii sheria ya HIPAA. Meta haitawajibikia Maelezo Yaliyopigwa Marufuku chini ya Makubaliano haya, bila kuzingatia chochote kile kilicho hapa ambacho kina kinzana.
    4. Kufidia. Utatetea, kuondolea lawama Meta (na Washirika wake na wakurugenzi wake, maafisa, wafanyakazi, mawakala na wawakilishi) dhidi ya madai yote (kutoka kwa kampuni nyingine na/au Watumiaji), gharama, hasara, wajibu na gharama (ikiwemo ada inayofaa ya kulipa wakili) yanayotokana na au kuhusiana na ukiukaji au madai ya ukiukaji wa Sehemu ya 2 au vinginevyo inavyohusiana na Data Yako, Sera Zako au matumizi ya Workplace yanayokiuka Makubaliano haya. Meta inaweza kushiriki katika kutetea na kuamua madai yoyote kama hayo kwa uamuzi na gharama yake binafsi. Hutagharamia dai lolote bila kibali kilichoandikwa awali kutoka Meta ikiwa kugharamia huko kutahitaji Meta kuchukua hatua yoyote, epuka kuchukua hatua yoyote au kukubali wajibu wowote.
    5. Nakala rudufu na Ufutaji wa Data. Meta haitoi huduma yoyote ya uhifadhi na unawajibikia uundaji wa nakala rudufu kwa Data Yako. Unaweza kufuta Data Yako inayojumuisha maudhui ya Mtumiaji wakati wowote wakati masharti yanatumika kupitia kipengele cha msimamizi wa mfumo katika Workplace.
    6. Jumla ya Data. Chini ya makubaliano haya, tunaweza pia kuzalisha data jumuishi ya takwimu na uchanganuzi unatokana na matumizi yako ya Workplace (“Data Jumuishi”), lakini Data Jumuishi kama hiyo haitajumuisha Data Yako au data yoyote ya kibinafsi.
  3. Usalama wa Data
    1. Usalama wa Data yako. Tutatumia hatua zifaazo za kiufundi, kishirika na kiusalama zilizoundwa ili kulinda Data Yako tuliyo nayo dhidi ya kufikiwa bila idhini, kubadilishwa, kutolewa au kuharibiwa kama ilivyofafanuliwa zaidi kwenye Kiongezo cha Usalama wa Data.
    2. Utoaji data Kisheria na Maombi ya Kampuni Nyingine. Kijumla unawajibikia kujibu maombi ya wahusika wengine kuhusu Data Yako, kama vile kutoka kwa wadhibiti, Watumiaji au shirika la kutekeleza sheria (“Maombi ya Wahusika Wengine”), lakini unaelewa kwamba, katika kujibu Ombi la Wahusika Wengine, Meta inaweza kutoa Data Yako ili kuzingatia mahitaji yake ya kisheria. Katika hali kama hizo, kadri tunavyoruhusiwa na sheria na masharti ya Ombi la Wahusika Wengine, tutatumia juhudi zifaazo ili (a) kukuarifu kuhusu kupokea kwetu kwa Ombi la Mshirika Mwingine na kumuuliza mhusika huyo kuwasiliana nawe na (b) tutazingatia maombi yako faafu kuhusu juhudi zako za kukataa Ombi la Mhusika Mwingine bila wewe kuhusishwa. Kwanza utahitajika kupata maelezo yanayohitajika kujibu Ombi la Kampuni Nyingine wewe binafsi na utawasiliana nasi tu ikiwa hutaweza kupata maelezo kama hayo.
  4. Malipo
    1. Ada. Unaweza kulipa Meta ada za kawaida za Workplace (ambazo kwa sasa zinapatikana: https://www.workplace.com/pricing) kwa matumizi yako ya Workplace, kwa kutegemea kipindi chochote cha jaribio kama ilivyofafanuliwa katika Sehemu ya 4.f (Jaribio la Bila Malipo), isipokuwa kama kuna makubaliano vinginevyo kwenye waraka ulioandikwa na kutiwa sahihi. Ada zote chini ya Makubaliano haya yatalipwa kwa USD, isipokuwa kama imebainishwa kwenye bidhaa, au isipokuwa kama kuna makubaliano vinginevyo kwenye waraka ulioandikwa na kutiwa sahihi. Ada zote zitalipwa zote kulingana na njia yako ya malipo kwa mujibu wa Sehemu ya 4.b. Malipo yoyote yatakayochelewa kufanywa yatatozwa ada za huduma sawa na asilimia 1.5% kila mwezi ya kiasi cha pesa kinachofaa kulipwa au kiasi cha juu zaidi kinachokubalika kisheria, kiasi kitakacho kuwa cha chini.
    2. Njia za Malipo. Unapoingia kwenye Makubaliano haya, unakubali kulipa ada chini ya mojawapo kati ya kategoria mbili za malipo: (i) mteja anayetumia kadi (iwe analipa moja kwa moja, au kupitia jukwaa la malipo la mtu mwingine), au (ii) mteja wa anayetumiwa ankara, kama ilivyobainishwa kwa uamuzi wa Meta. Wateja wanaotumia kadi wanaweza (kwa Uamuzi binafsi wa Meta) kuwa wateja wa kutumiwa ankara (au vinginevyo) kwa misingi kama vile idadi ya Watumiaji na uwezo wao wa kushughulikia mikopo, lakini Meta inasalia na haki ya kukuweka upya katika kategoria kama mteja anayetumia kadi au mteja wa kutumiwa ankara.
      1. Wateja Wanaotumia Kadi Kulipa. Wateja wanaotumia kadi kulipa watatozwa kwenye kadi zao malipo kwa matumizi ya Workplace.
      2. Wateja wanaotumiwa Ankara. Wateja wanaotumiwa Ankara watapewa muda wa mkopo na Meta na watapewa ankara kila mwezi, isipokuwa kama kumefanywa mabadiliko vinginevyo kwenye waraka ulioandikwa na kutiwa sahihi. Ikiwa utawekwa katika kategoria ya wateja wanaotumiwa Ankara, utalipa ada zote hitajika chini ya Makubaliano haya, kikamilifu na kulipa pesa zote ilivyoagizwa nasi ndani ya siku 30 ya tarehe ya kuwekwa Ankara.
      3. Unakubali kwamba tunaweza kuchukua ripoti ya mkopo ya kampuni yako kutoka kwenye taasisi inayosimamia mikopo unapokubali Makubaliano haya au wakati wowote baadaye.
    3. Ushuru. Ada zote zimetajwa bila kujumuisha ushuru wowote unaotumika na unahitajika kulipa na kuwajibikia mauzo, matumizi, GST, thamani iliyoongezwa, kushikiliwa kwokwote au ushuru sawia au kodi, uwe ni wa ndani au kimataifa, unaohusiana na miamala chini ya Makubaliano haya, kando na ushuru kwa msingi wa mapato ya Meta. Utalipa pesa zote zinazohitajika chini ya Makubaliano haya bila kudai kufidiwa, kuondolewa kwa kiasi fulani au kusalia na kiasi fulani. Ikiwa malipo yoyote utakayofanya chini ya Makubaliano haya yatahitaji kuondolewa kiasi fulani au kiasi fulani kusalia, utawajibika kufanya malipo yafaayo kwa mamlaka ifaayo ya ushuru na utawajibikia riba, adhabu, faini, au wajibu kama huo wa kifedha unaotaokana na wewe kutotuma ushuru kama huo kwa mamlaka au shirika lifaalo la kiserikali. Unakiri na kukubali kuwa unafikia na kutumia Workplace kwa kutumia anwani ya malipo iliyorodheshwa kwenye Makubaliano haya au vinginevyo umetutumia andiko na ikiwa anwani kama hiyo ni ya Marekani, tutakutoza ushuru unaotumika nchini Marekani wa ununuzi/matumizi kulingana na eneo la anwani yako ya malipo. Ikiwa mamlaka inayosimamia ushuru katika jimbo fulani la Marekani itasema kwamba Meta ingepaswa kukusanya ushuru kutoka kwako, na ulilipa ushuru kama huo moja kwa moja kwa serikali, unakubali kutupa ushahidi kwamba ushuru kama huo ulilipwa (kwa kuridhisha mamlaka kama hiyo ya ushuru) ndani ya siku thalathini (30) baada ya Meta kutuma ombi lililoandikwa. Unakubali kutuondolea lawama ikiwa kuna malipo ya chini au kutolipwa kwa ushuru, adhabu na riba.
    4. Kusitishwa. Bila kuathiri haki zetu zozote chini ya Makubaliano haya, ikiwa hutalipa ada zozote kufikia tarehe ya kufanya malipo, basi tutasitisha ama huduma yote au sehemu ya Workplace (ikijumuisha uwezo wa kufikia huduma zinazolipiwa) hadi pale malipo yafanywe kikamilifu.
    5. Workplace kwa ajili ya Ufikiaji Bora bila Malipo. Licha ya Sehemu ya 4.a, ukituma ombi la ufikiaji wa bila malipo chini ya programu ya Workplace for Good na Meta ibaini kwamba umehitimu kulingana na sera za Meta (ambazo kwa sasa zimerejelewa katika https://work.workplace.com/help/work/142977843114744) tutatoa Workplace kwako bila kukutoza kulingana na sera kama hizo kwa msingi wa kuendelea. Ikiwa hutahitimu tena kupata ufikiaji bila malipo kutokana na mabadiliko kwenye sera zetu, basi Meta itakutumia notisi miezi mitatu (3) kabla kuhusu hili na baada ya notisi kama hiyo, Sehemu ya 4.a itatumika.
    6. Jaribio la Bila malipo. Meta inaweza kutoa jaribio la bila malipo la Workplace kwa kipindi kamili kwa uamuzi wake binafsi, kipindi ambacho Meta itabaini kwa uamuzi wake binafsi na kukujulisha kupitia kidirisha cha msimamizi ya toleo lako la Workplace. Mwisho wa kipindi kama hicho cha jaribio la bila malipo, Sehemu ya 4.a (Ada) zitatumika.
  5. Usiri
    1. Majukumu. Kila mhusika anakubali kwamba maelezo yote ya kibiashara, kiufundi na kifedha watakayopokea (kama “Mhusika Mpokeaji”) kutoka kwa mhusika anayetoa maelezo kuhusiana na Makubaliano haya (“Mhusika Mtoaji Maelezo”) yanajumuisha mali ya siri ya Mhusika Mtoaji Maelezo (“Maelezo ya Siri”), alimradi yametambulishwa kuwa ama ya siri au ya mali ya akili wakati wa utoaji au yanapaswa kufahamiwa ifaavyo na Mhusika Mpokeaji kuwa ni ya siri au ni mali ya akili kutokana na hali ya maelezo yanayotolewa na hali zinazozingira utoaji wake. Isipokuwa kama ilivyoidhinishwa hapa, Mhusika Mpokezi (1) ataweka Maelezo ya Siri yawe siri na hatatoa maelezo hayo kwa kampuni nyingine na (2) hatatumia Maelezo ya Siri kwa madhumuni yoyote kando na kutimiza wajibu wake na kutekeleza haki zake chini ya Makubaliano haya. Mhusika Mpokeaji anaweza kutoa Maelezo ya Siri kwa wafanyakazi wake, wakala, wanakandarasi na wawakilishi wengine akiwa na hitaji halali ya kufahamu (ikiwemo, kwa Meta, yale ya Washirika wake na wanakandarasi wengine waliorejelewa katika Sehemu ya 11.j), alimradi wanazingatia wajibu wa usiri usio pungua ulinzi wa Maelezo ya Siri ya Mhusika Anayetoa Maelezo kama ilivyobainishwa katika Sehemu ya 5 na kwamba Mhusika Mpokeaji asalie kuwajibikia uzingatifu wa mtu yeyote kama huyo wa masharti ya Sehemu ya 5.
    2. Hali Maalum. Wajibu wa Mhusika Mpokezi wa kuweka siri hautatumika katika maelezo ambayo Mhusika Mpokezi anaweza kuthibitisha kwa hati kuwa: (a) alikuwa nayo kihalali au kufahamu kuyahusu kabla yake kupokea Maelezo ya Siri; (b) yamejulikana kwa umma lakini si kwa kosa lake Mhusika Mpokezi; (c) yamepokewa kihalali naye Mhusika Mpokezi kutoka kwa mshirika mwingine bila kukiuka wajibu wowote wa siri; au (d) yamekuzwa na wafanyakazi wa Mhusika Mpokezi ambao hawana idhini ya kufikia maelezo kama hayo. Mhusika Mpokezi anaweza kutoa maelezo kadri inavyohitajika Kisheria au na koti, alimradi (isipokuwa ikipigwa marufuku Kisheria) Mhusika Mpokezi anaarifu Mhusika Mtoaji Maelezo kwa wakati ufaao na anashirikiana katika jitihada zozote za kutaka kushughulikiwa kisiri.
    3. Afueni ya Korti. Mhusika Mpokezi anakiri kuwa matumizi ya au kutoa Maelezo ya Siri kwa kukiuka Sehemu hii ya 5 kunaweza kusababisha madhara makubwa ambayo hayawezi kusuluhishwa kwa fidia pekee na kwa hivyo anakiri kwamba endapo matumizi halisi au yanayotishiwa au Mhusika Mpokezi anapotoa maelezo, Mhusika mtoaji Maelezo anaweza kutafuta afueni ufaao pamoja na suluhu nyingine yoyote anaweza kupata kisheria.
  6. Haki Miliki
    1. Umiliki wa Meta. Haya ni makubaliano ya kufikia na kutumia Workplace na hakuna haki miliki zozote zinazopewa Mteja. Meta na watoaji leseni wake wanabakiza haki zote, hadhi na matakwa (zikiwemo haki zote za umiliki) kwenye na kwa Workplace, Data Jumla na teknolojia yoyote husika, na kazi zozote zalishi, mabadiliko au kuboreshwa kwa maelezo haya yaliyoundwa na au kwa niaba ya Meta, ikiwa ni pamoja na kulingana na Maoni yako (yalivyofafanuliwa hapa chini). Hakuna haki zozote unazopewa isipokuwa ilivyoelezwa moja kwa moja kwenye Makubaliano haya.
    2. Maoni. Ikiwa utawasilisha maoni, maswali, mapendekezo, mifano ya matumizi au maoni mengine yanayohusiana na matumizi yako ya Workplace au programu zake za API au bidhaa au huduma zetu nyingine (“Maoni”), tunaweza kutumia Maoni kama hayo kuhusiana na bidhaa au huduma zetu zozote au za Washirika wetu, bila kuwajibikia au kukufidia.
  7. Kikanusho
    META INAKANUSHA DHAMANA ZOZOTE NA ZOTE NA UWAKILISHO WA AINA YOYOTE WA MOJA KWA MOJA, UNAOKISIWA AU WA MAKUBALIANO, ZIKIWEMO DHAMANA ZA UWEZO WA KUUZA, UFAAFU KWA AJILI YA LENGO FULANI, HAKI AU KUTOINGILIA. HATUTOI HAKIKISHO KWAMBA WORKPLACE HAITAKUMBWA NA MATATIZO AU ITAKOSA HITILAFU. TUNAWEZA KURUHUSU WAHUSIKA WENGINE KUUNDA NA KUTOA HUDUMA NA PROGRAMU AMBAZO ZINAJAZILIA MATUMIZI YAKO YA WORKPLACE AU TUNAWEZA KURUHUSU WORKPLACE VINGINEVYO KUJUMUISHWA NA HUDUMA NA PROGRAMU NYINGINE. META HAIWAJIBIKII HUDUMA AU PROGRAMU AMBAZO UTACHAGUA KUTUMIA KUHUSIANA NA WORKPLACE. MATUMIZI YAKO YA HUDUMA AU PROGRAMU KAMA HIZO YANALINGANA NA MASHARTI NA SERA TOFAUTI NA UNAKIRI NA KUKUBALI KWAMBA MATUMIZI YOYOTE NI KWA TAHADHARI YAKO.
  8. Vikwazo vya Wajibu
    1. ISIPOKUWA KWA MADAI AMBAYO HAYAJAJUMUISHWA (ILIVYOFAFANULIWA HAPA CHINI):
      1. HAKUNA MHUSIKA ATAKAYEWAJIBIKIA HASARA YOYOTE YA MATUMIZI, DATA ILIYOPOTEA AU ISIYO SAHIHI, KUSITISHWA KWA BIASHARA, GHARAMA YA KUCHELEWA AU HASARA YOYOTE ISIYO YA MOJA KWA MOJA AU INAYOFUATIA JAMBO LOLOTE LILE (ZIKIWEMO KUPOTEA KWA FAIDA), BILA KUJALI NAMNA YA HATUA, IWE KATIKA KANDARASI, UKIUKAJI WA HAKI (UKIWEMO UZEMBE), KANUNI KALI ZA UWAJIBIKAJI AU VINGINEVYO, HATA IKIWA WATAJULISHWA MAPEMA KUHUSU UWEZEKANO WA UHARIBIFU KAMA HUO; NA
      2. JUMLA YA WAJIBU WA MHUSIKA YEYOTE KWA MWENZAKE HAUTAZIDI KIASI HALISI KILICHOLIPWA AU UNAOWEZA KULIPWA NA MTEJA KWA META KATIKA KIPINDI CHA MIEZI (12) YA AWALI CHINI YA MAKUBALIANO HAYA AU IKIWA HAKUNA ADA ZINAZOLIPWA AU ZINAPASWA KULIPWA KATIKA KIPINDI KAMA HICHO, DOLA ELFU KUMI ($10,000).
    2. Kwa madhumuni ya Sehemu hii ya 8, “Madai ambayo Hayajajumuishwa” yana maana ya: (a) Wajibu wa mteja unaotokana na Sehemu ya 2 (Data yako na Wajibu wako”); na (b) ukiukaji wa wajibu wa mhusika katika Sehemu ya 5 (Usiri) lakini bila kujumuisha madai yanayohusiana na Data Yako.
    3. Vikwazo vilivyo katika Sehemu ya 8 vitadumu na kutumika hata ikiwa suluhu yoyote iliyodhibitiwa iliyobainishwa katika Makubaliano haya itashindwa kutimiza madhumuni yake msingi, na wahusika wakubali kwamba hakuna mhusika ambaye anadhibiti au kutojumuisha wajibu wao kwa ajili ya kitu chochote kisichoweza kuwekewa vikwazo au kutojumuishwa kisheria. Unakiri na kukubali kwamba kutoa kwetu huduma ya Workplace kumeegemezwa katika msingi kwamba uwajibikaji wetu umewekewa vikwazo kama ilivyo kwenye Makubaliano haya.
  9. Kipindi na Utamatishaji
    1. Kipindi. Makubaliano haya yataanza kutumika katika tarehe ambapo utafikia toleo lako la Workplace kwa mara ya kwanza na kuendelea hadi kusitishwa kama ilivyoruhusiwa hapa katika “Masharti”).
    2. Kusitishwa ili kulinda Masilahi. Bila kupuuza haki zako za kutamatisha chini ya aya ya 2.d ya Kiambatisho cha Uchakataji Data, unaweza kutamatisha Makubaliano haya wakati wowote, bila au kwa sababu yoyote, baada ya kuandika ilani siku 30 mapema kwa Meta na msimamizi wako aliyeteua kufuta toleo lako la Workplace ndani ya bidhaa. Meta pia inaweza kutamatisha Makubaliano haya wakati wowote, bila au kwa sababu yoyote baada yake kukuandikia ilani siku 30 kabla ya kufanya hivyo.
    3. Meta Kusitisha na Kutamatisha. Meta inasalia na haki ya kusitisha Makubaliano haya kwa kukuandikia ilani ifaayo au kufunga ufikiaji wako kwa Workplace ikiwa utakiuka Makubaliano haya au ikiwa tutachukulia hatua kama hiyo kuwa muhimu katika kuzuia madhara ya kiusalama, uthabiti, upatikanaji au uadilifu wa Workplace.
    4. Kufutwa kwa Data Yako. Meta itafuta Data Yako haraka iwezekanavyo baada ya utamatishaji wowote wa Makubaliano haya, lakini unaelewa kwamba maudhui yaliyofutwa yatasalia kwenye nakala rudufu kwa muda ufaao huku mchakato wa ufutaji ukiendelea. Kama ilivyoelezwa katika Sehemu ya 2.e, unawajibikia kuundwa kwa nakala zozote rudufu ya Data Yako kwa malengo yako binafsi.
    5. Athari ya Kusitishwa. Baada ya kutamatishwa kwa Makubaliano haya: (a) wewe pamoja na Watumiaji wako lazima mwache kutumia Workplace mara moja; (b) baada ya kupokea ombi kutoka kwa Mhusika Mtoaji maelezo, na kulingana na sehemu ya 9.d, Mhusika Mpokeaji maelezo atarejesha au kufuta Maelezo yoyote ya Siri ya Mhusika Anayeyatoa aliyo nayo mara moja; (c) utalipa Meta ada zozote ambazo hazijlipwa ambazo ulitumia kabla ya kutamatishwa huku; (d) ikiwa Meta itasitisha Makubaliano haya bila sababu kulingana na sehemu ya 9.b, Meta itakurejeshea kiasi linganifu cha ada zozote zilizolipwa mapema (panapohitajika); na (e) Sehemu zifuatazo zitadumu: 1.c (Vikwazo), 2 (Matumizi ya Data Yako na Wajibu Wako) (kando na leseni ya Meta kwa Data Yako katika Sehemu ya 2.a), 3.b (Utoaji maelezo kisheria na Maombi ya Wahusika Wengine), 4 (Malipo) kupitia 12 “(Ufafanuzi). Isipokuwa kama ilivyobainishwa kwenye Makubaliano haya, mhusika yeyote akitekeleza suluhu yoyote, ikiwa ni pamoja kusitisha huduma, atafanya hivyo bila kupuuza suluhu nyingine anayoweza kuwa anatekeleza chini ya Makubaliano haya kisheria au vinginevyo.
  10. Akaunti Nyingine za Facebook.
    1. Akaunti za Kibinafsi. Ili kuepuka tashwishi, Akaunti za Mtumiaji ni tofauti na akaunti ya kibinafsi ya Facebook ambazo Watumiaji wanaweza kuunda katika huduma ya mtumiaji Facebook (“Akaunti za kibinafsi za FB”). Akaunti za kibinafsi za FB hazizingatii Makubaliano haya lakini badala yake zinazingatia masharti ya Meta kwa huduma hizo, kila mojawapo kati ya Meta na Mtumiaji anayefaa.
    2. Workplace na Matangazo. Hatutaonyesha kampuni nyingine wanaotangaza kwenye huduma ya Workplace ya Watumiaji wako na hatutatumia Data Yako kutoa au kuwalenga Watumiaji wako na matangazo au kubinafsisha matumizi ya Watumiaji wako kwenye Akaunti zao za Kibinafsi. Meta inaweza, hata hivyo, kufanya matangazo ya ndani ya bidhaa au kujulisha wasimamizi wa mfumo kuhusu vipengele, mijumuisho au zana zinahusiana na Workplace.
  11. Jumla
    1. Mabadiliko. Meta inaweza kubadilisha masharti ya Makubaliano haya na sera zilizorejelewa kwenye au zilizojumuishwa kwenye Makubaliano haya wakati wowote, ikiwemo wala sio tu Kiambatisho cha Uchakataji Data na Kiambatisho cha Uhamishaji wa Data (ili kuzingatia sheria tumika za ulindaji data), Kiambatisho cha Usalama wa Data na Sera Kubalifu ya Matumizi, kwa kukupa arifa kupitia barua pepe, kupitia huduma au kwa njia nyingine faafu (“Mabadiliko”). Kwa kuendelea kutumia Workplace siku 14 baada ya ilani yetu, unakubali Mabadiliko kama hayo.
    2. Sheria Tawala. Makubaliano haya na matumizi yako na ya Watumiaji wako ya Workplace pamoja na dai lolote linaloweza kuibuka kati yako nasi, linatawaliwa na, na lazima yafasiriwe kwa mujibu wa sheria za Marekani na jimbo la Kalifonia, invyotumika, bila kuangazia athari ya misingi yao ya mikinzano ya sheria. Dai au sababu yoyote ya hatua inayotokana na au kuhusiana na Makubaliano haya au Workplace lazima ianzishwe nchini Marekani pekee. Mahakama ya Wilaya ya Wilaya ya Kaskazini ya California au mahakama ya jimbo inayopatikana katika Jimbo la San Mateo, na kila mhusika anakubali mamlaka ya kibinafsi ya mahakama kama hizo.
    3. Makubaliano Yote. Makubaliano haya (yanayojumuisha Sera Kubalifu ya Matumizi) ndiyo makubaliano kamilifu kati ya wahusika kuhusiana na ufikiaji wako wa na matumizi ya Workplace na hupiku mawakilisho au makubaliano yoyote ya awali yanayohusiana na Workplace. Vichwa vinatumika katika masilahi fulani tu, na istilahi kama vile “inajumuisha” zinafaa kutafsiriwa bila vikwazo. Makubaliano haya yameandikwa kwa Kiingereza (cha Marekani), na yatatumika kuamua mikinzano kwenye toleo lolote lilolotasiriwa.
    4. Msamaha na Kiwango cha athari yake. Kutotekelezwa kwa masharti hakutachukuliwa kuwa ni msamaha; Misamaha lazima iandikwe na itiwe sahihi na mhusika anayedai kusamehewa. Masharti au sheria zozote katika oda ya ununuzi ya Mteja au fomu ya biashara haitabadilisha Makubaliano haya na zimekataliwa hapa moja kwa moja na hati kama hizo zitatumika kwa malengo ya kiutawala tu. Ikiwa masharti yoyote kwenye Makubaliano haya yataamuliwa na korti yenye hadhi ya umilisi kuwa hayawezi kutekelezwa, si sahihi au vinginevyo yanakiuka sheria, masharti kama hayo yatafsiriwa ili kutimiza malengo yako yake lengwa huku masharti mengine yaliyosalia kwenye Makubaliano haya yakiendelea kutumika kikamilifu.
    5. Habari kwa Umma. Taarifa yoyote kwa vyombo vya habari au kampeni ya uuzaji kuhusu mahusiano ya wahusika zinahitaji wahusika wote wawili kuidhinisha mapema kwa maandishi. Licha ya hayo: (a) ndani ya kampuni yako binafsi, unaweza kutangaza au kuendeleza matumizi ya Workplace katika kipindi ambapo Masharti yanatumika (mfano, ili kuhimiza Watumiaji kuanza kutumia), kulingana na miongozo ya Meta ya matumizi inayotolewa muda baada ya muda na (b) Meta inaweza kurejelea jina na hali yako kama mteja wa Workplace.
    6. Kazi. Wahusika wote hawawezi kukabidhi Makubaliano haya au haki zake au majukumu yake nchini ya Makubaliano haya bila kibali kilichoandikwa mapema kutoka kwa mhusika mwingine, isipokuwa kwamba Meta inaweza kukabidhi Makubaliano haya bila kibali cha Washirika wake wowote au kuhusiana na muungano, upangaji upya, ununuzi au kuhamisha wa mali zake zote au zile muhimu zote au dhamana ya upigaji kura katika uteuzi. Kutokana na haya yaliyoelezwa hapa juu, Makubaliano haya yanawafumbata na kutumika kwa manufaa ya kila warithi na wakabidhiwa walioidhinishwa rasmi wa mhusika. Wakabidhiwa ambao hawajaidhinishwa wamepigwa marufuku na hawataunda wajibu wowote kwenye Meta.
    7. Wanakandarasi Huru. Wahusika wote ni wanakandarasi huru. Hakuna kampuni, ushirika, biashara ya pamoja au nafasi ya kazi inayoundwa kutokana na Makubaliano haya na hakuna mhusika anaye na mamlaka ya kumfumbata mwenzake.
    8. Hakuna Manufaa kwa Kampuni Nyingine. Makubaliano haya yananufaisha Meta na Mteja na hailengi kuwanufaisha wahusika wengine, wakiwemo Watumiaji wowote.
    9. Ilani. Pale ambapo unatamatisha Makubaliano haya kwa mujibu wa Sehemu ya 9.b, ni sharti uarifu Meta kupitia msimamizi wako wa mfumo aliyeteua kufuta toleo lako la Workplace ndani ya bidhaa. Notisi yoyote nyingine chini ya Makubaliano haya lazima yawe kwa maandishi, ambayo lazima yatumwe kwa Meta kupitia anwani ifuatayo (kama inavyotumika:) katika kesi ya Meta Platforms Ireland Ltd, kwa 4 Grand Canal Square, Dublin 2, Ireland, Umakinifu: Legal na, ikiwa ni Meta Platforms Inc, kwa 1 Hacker Way, Menlo Park, CA 94025 USA, Umakinifu: Kisheria. Meta inaweza kutuma ilani kwenye anwani ya barua pepe iliyo katika akaunti ya Mteja. Meta pia inaweza kutoa ilani za kiutendakazi kuhusu Workplace au ilani nyingine za kibiashara kupitia ujumbe kwa Wateja ndani ya Workplace au machapisho bayana kwenye Workplace.
    10. Wanakandarasi wadogo. Meta inaweza kutumia wanakandarasi wadogo na kuwaruhusu kutekeleza haki za Meta chini ya Makubaliano haya, lakini Meta inasalia na wajibu wa kuhakikisha kila mwanakandarasi mdogo kama huyo anazingatia Makubaliano haya.
    11. Tukio lisilo la kawaida ka kuzuia kufuata mkataba. Hakuna mshirika atakayewajibikia mwenzake kutokeapo kuchelewa au kutotekelezwa kwa wajibu wowote chini ya Makubaliano haya (isipokuwa katika kutolipwa kwa ada) ikiwa kuchelewa huko kunatokana na matukio yasiyotabirika yanayofanyika baada ya kutia sahihi Makubaliano haya na yale ambayo hayawezi kuepukika na mhusika kama huyo, kama vile migomo, kuzuiwa, vita, vitendo vya kigaidi, fujo, majanga ya asili, kupotea au kupungua kwa nguvu za umeme au mawasiliano ya simu au data za mitandao au huduma, au shirika la serikali kukataa kutoa leseni au idhini.
    12. Tovuti za Kampuni Nyingine. Workplace inaweza kuwa na viungo vya kuelekeza kwenye tovuti za kampuni nyingine. Hii haina maana kwamba tunapigia upato tovuti yoyote na hatuwajibikii matendo, maudhui, maelezo au data yoyote ya tovuti za kampuni nyingine au matendo au viungo vyovyote vilivyomo kwenye tovuti hizo au mabadiliko au visasisho yoyote kwazo. Tovuti za kampuni nyingine zinaweza kutoa sheria na masharti yao binafsi ya matumizi na sera za faragha zinazotumika kwako na Watumaji wako na matumizi yako ya tovuti za kampuni nyingine hayadhibitiwi na Makubaliano haya.
    13. Vidhibiti vya Uhamishaji Bidhaa na Vikwazo vya Kibiashara. Katika kutumia Workplace, Mteja anakubali kuzingatia sheria na kanuni za Marekani kuhusu uuzaji na ununuzi kutoka nchi nyingine na sheria nyingine zinazotumika sawa na vikwazo vyovyote au vizuizi vya kibiashara vinavyotumika. Bila kuwekea vikwazo mambo hayo hapo juu, Mteja anawakilisha na kudhamini kwamba: (a) hajaorodheshwa katika orodha ya serikali ya Marekani inayopiga marufuku au kuwekea wahusika vikwazo; (b) hahusiki katika vikwazo vya kiuchumi au vikwazo vya biashara vya Umoja wa Mataifa, Marekani, Umoja wa Ulaya au vikwazo vingine vyovyote; na (c) haendelezi kazi zake au haina Watumiaji katika nchi inayozingatia vikwazo kamilifu vya kibiashara vya Marekani.
    14. Masharti kuhusu Matumizi kwa Mashirika ya Kiserekali. Ikiwa wewe ni Shirika la Kiserekali, unawakilisha kwamba: (i) hakuna sheria tumika, sera, au kanuni inayokuwekea vikwazo dhidi ya kukubali na kutenda au kukubali utendaji wa sharti au kanuni yoyote ya Makubaliano haya, (ii) hakuna sheria tumika, sera au kanuni inayofanya sharti au kanuni yoyote ya Makubaliano haya kutoweza kutekelezwa dhidi yako au Shirika Lolote tumika la Kiserekeli, (iii) una idhini ya na una uwezo wa kisheria chini ya sheria tumika, sera na kanuni ya kuwakilisha na kujumuisha Shirika lolote la Kiserekali kwenye Makubaliano haya; na (iv) unaingia katika Makubaliano haya kwa msingi wa uamuzi yakinifu kuhusiana na thamani ya Workplace kwako na Watumiaji wako na hakuna kitendo au mgongano wa mapendeleo usiofaa ambao ulichochea uamuzi wako wa kuingia katika Makubaliano haya. Usiingie katika Makubaliano haya ikiwa huwezi kuwakilisha yaliyomo katika Sehemu ya 11.n. Ikiwa Shirika la Kiserikali litaingia katika Makubaliano kwa kukiuka Sehemu hii ya 11.n, Meta inaweza kuteua kutamatisha Makubaliano haya.
    15. Wauzaji upya. Unaweza kuchagua kufikia na kutumia Workplace kupitia Muuzaji upya. Endapo utafikia na kutumia Workplace kupitia Muuzaji upya, Unawajibu wa kibinafsi kwa: (i) haki na wajibu wowote unaohusiana katika makubaliano tumika na Muuzaji upya huyo, na (ii) kati yako na Meta, ufikiaji wowote wa Muuzaji tena kwa toleo lako la Workplace, Data Yako na akaunti zozote za Mtumiaji ambazo huenda umeunda kwa ajili ya Muuzaji upya wako. Vilevile, ikiwa utachagua kufikia na kutumia Workplace kupitia Muuzaji upya, unakubali kwamba Masharti ya Mteja wa Muuzaji upya yatatawala masharti yoyote yanayogongana katika Makubaliano haya.
  12. Ufafanuzi
    Katika Makubaliano haya, isipokuwa ikielezwa vinginevyo:
    "Sera Zinazokubalika za Matumizi" ina maana ya kanuni za matumizi ya Workplace zinazopatikana katika www.workplace.com/legal/FB_Work_AUP, kama zinavyoweza kubadilishwa muda baada ya muda.
    Mshirika” inamaanisha shirika ambalo humiliki au kudhibiti moja kwa moja au vinginevyo, linamilikiwa au linadhibitiwa na au linamilikiwa au kudhibitiwa kwa pamoja na kampuni fulani, ambapo “udhibiti” una maana ya uwezo wa kuelekeza usimamizi au kazi za shirika, na “umiliki” una maana umiliki wenye manufaa wa 50% (au, ikiwa sheria tumika hairuhusu umiliki wa wengi, idadi ya juu zaidi inayokubalika chini ya sheria kama hiyo) au zaidi ya usalama wa usawa wa kupiga kura kwa shirika au mapendeleo sawa ya kupiga kura. Kwa ajili ya ufafanuzi huu, Shirika la Kiserekali sio mshirika wa Shirika lingine la Kiserekali isipokuwa inapodhibiti kikamilifu Shirika kama hilo la Kiserikali.
    Kiambatisho cha Uchakataji Data” ina maana ya kiambatisho cha uchakataji data kilichoambatishwa kwenye, na kinakuwa sehemu ya, Makubaliano haya, ikijumuisha masharti yoyote yaliyorejelewa humo.
    Kiambatisho cha Usalama wa Data” ina maana ya kiongezo cha usalama wa data kilichoambatishwa kwenye na kuwa sehemu ya Makubaliano haya.
    Shirika la Kiserikali” ina maana ya taifa lolote au eneo ulimwenguni, ikiwa ni pamoja wala sio tu jimbo lolote, eneo la mtaani, manispaa, kanda au vitengo vingine au maeneo madogo ya kisiasa ya serikali, shirika lolote la kiserikali, shirika, biashara au mashirika mengine yaliyoendelea, yanayomilikiwa au kudhibitiwa na serikali kama hizo, na mwakilishi yeyote au ajenti wa asasi zilizoelezwa hapo juu.
    Sheria” ina maana ya sheria tumika za mtaani, jimbo, eneo au za kimataifa, kanuni na mikataba, ikiwemo wala sio tu ile inayohusiana na faragha na uhamishaji wa data, mawasiliano ya kimataifa, uhamishaji wa data ya kiufundi au ya kibinafsi na ununuzi wa umma.
    Muuzaji upya” ina maana ya mhusika mwingine ambaye ana makubaliano halali na Meta yanayoidhinisha kuuza tena na kuwezesha ufikiaji wa Workplace.
    "Masharti ya Mteja Muuzaji upya" ina maana ya masharti yanayopatikana katika https://www.workplace.com/legal/FB_Work_ResellerCustomerTerms, kama yanavyosasishwa muda baada ya muda na kuunda sehemu ya Makubaliano haya na kuwa masharti ya ziada yanayotumika kwako kati ya wahusika, iwapo unafikia na kutumia Workplace kupitia Muuzaji upya.
    "Watumiaji" ina maana ya wafanyakazi wowote wa Washirika wako, wanakandarasi au watu wengine ambao unawaruhusu kufikia Workplace.
    Workplace” ina maana ya huduma ya Workplace tunayokupa chini ya Makubaliano, haya na matoleo yoyote yale yatakayofuata, zikiwemo tovuti, programu, huduma za mtandaoni, zana na maudhui yoyote ambayo huenda tukakupa chini ya Makubaliano haya, kama inavyoweza kurekebishwa muda baada ya muda.
    Data Yako” ina maana ya (a) maelezo yoyote ya anwani au data ya kusajili mtandao aua akaunti ambayo wewe au Watumiaji wako wanatoa kwa Workplace; (b) maudhui au data yoyote ambayo wewe au Watumiaji wako wanachapisha, kushiriki, kuhamisha au kutoa kwenye Workplace; (c) maelezo ambayo unakusanya wakati wewe na Watumiaji wako wanawasiliana nasi kwa ajili ya usaidizi unaohusiana na Workplace, yakiwemo maelezo kuhusu vifaa, programu na maelezo mengine yanayokusanywa yanayohusiana na kipengele cha usaidizi; na (d) matumizi yoyote au maelezo msingi (m.f anwani za IP, kivinjari na aina nyingine za mfumo wa uendeshaji na vitambuzi vya kifaa) yanayohusu mtagusano wa Watumiaji na Workplace.
    Sera Zako” ina maana ya sera tumika za mfanyakazi, mifumo, faragha, Idara ya Uajiri, malalamishi au sera nyingine.







Kiambatisho cha Uchakataji wa Data

  1. Ufafanuzi
    Ndani ya Kiambatisho hiki cha Uchakataji Data, “GDPR” ina maana ya Kanuni ya Kawaida ya Ulindaji Data (Kanuni ya (EU) 2016/679), na maneno haya “Mdhibiti”, “Mchakataji Data”, “Mhusika wa Data”, “Data ya Kibinafsi”, “Ukiukaji wa Data Binafsi” na “Uchakataji” yatakuwa na maana sawa kama yalivyofafanuliwa katika GDPR. “Imechakatwa” na “Chakata” yataeleweka kulingana na ufafanuzi kuhusu maana ya “Uchakataji”. Marejeleo ya GDPR na utoleaji wake yanajumuisha GDPR ilivyorekebishwa na kuingizwa kwenye sharia ya Uingereza. Istilahi nyingine zote zilizofafanuliwa hapa zitakuwa na maana sawa kama zilivyofafanuliwa kwingineko kwenye Makubaliano haya.
  2. Uchakataji wa Data
    1. Kwa kutekeleza shughuli zake kama Mchakataji chini ya Makubaliano haya kuhusiana na Data yoyote ya Kibinafsi kwenye Data Yako (“Data Yako ya Kibinafsi”), Meta inathibitisha kwamba:
      1. kipindi, mada, hali na madhumuni ya Uchakataji huu yatabainishwa kwenye Makubaliano haya;
      2. aina za Data ya Kibinafsi Zinazochakatwa zitajumuisha zile zilizobainishwa kwenye ufafanuzi wa Data Yako;
      3. kategoria za Wamiliki wa Data zinajumuisha wawakilishi wako, Watumiaji na watu wengine waliotambuliwa au wanaweza kutambulika kupitia Data Yako ya Kibinafsi; na
      4. majukumu na haki zako kama Mdhibiti Data kuhusiana na Data yako ya Kibinafsi zimeelezwa kwenye Makubaliano haya.
    2. Kwa kiwango ambacho Meta Huchakata Data yako ya Kibinafsi chini ya au kuhusiana na Makubaliano, Meta:
      1. itachakata tu Data yako ya Kibinafsi kulingana na maelezo yako kama yalivyoelezwa kwenye Makubaliano haya, ikiwa ni pamoja na kwa mujibu wa uhamishaji wa Data yako ya Kibinafsi, kwa kutegemea hali za kipekee zilizoruhusiwa chini ya Kifungu cha 28(3)(a) cha GDPR;
      2. itahakikisha kwamba wafanyakazi wake walio na idhini ya Kuchakata Data Yako ya Kibinafsi chini ya Makubaliano haya wameapa kuzingatia siri au wanadhibitiwa na sheria kuhusu majukumu ya kulinda siri kuhusiana na Data yako ya Kibinafsi;
      3. itatekeleza hatua za kiufundi na za kishirika zilizobainishwa kwenye Kiambatisho cha Usalama wa Data;
      4. itazingatia kanuni zinazorejelewa hapa chini kwenye Sehemu ya 2.c na 2.d ya Kiambatisho cha Uchakataji Data inapowateua Wachakataji- wa kiwango cha chini;
      5. itakusaidia kwa kukupa hatua zifaazo za kiufundi na za kishirika kadri hii inavyowezekana kupitia Workplace, ili kukuwezesha kutimiza wajibu wako wa kujibu maombi ya Mmiliki Data ya kutekeleza haki chini ya Sura ya III ya GDPR;
      6. itakusaidia kuhakikisha unazingatia majukumu yako kwa mujibu wa Kifungu cha 32 hadi 36 ya GDPR kwa kuzingatia hali ya Uchakataji na maelezo yanayotolewa kwa Meta;
      7. endapo Makubaliano yatasitishwa, Facebook, itafuta Data ya Kibinafsi kwa mujibu wa Mkataba isipokuwa endapo Umoja wa Ulaya au sheria za nchi mwanachama zitahitaji kwamba Data ya Kibinafsi ihifadhiwe;
      8. itakupa maelezo yote yaliyoelezwa kwenye Makubaliano haya na kupitia Workplace katika kutimiza majukumu ya Meta ya kutoa maelezo yote muhimu ili kuonyesha Meta inatii majukumu yake chini ya Kifungu cha 28 cha GDPR; na
      9. baada ya kila mwaka, Meta inakubali kwamba itachagua kampuni nyingine itakayoendesha shughuli ya ukaguzi ya SOC 2 Aina ya II au ukaguzi mwingine unaokubalika kitaaluma wa udhibiti wa Meta kuhusiana na Workplace, unazipa uwezo kikazi kampuni nyingine kama hizo. Ikiwa utaomba, Meta itakupa nakala ya ripoti ya ukaguzi ya wakati huo na ripoti kama hiyo itazingatiwa kuwa ni Maelezo ya Siri ya Meta.
    3. Unaidhinisha Meta kuwapa kandarasi ya majukumu ya Uchakataji data chini ya Makubaliano haya kwa Washirika wa Meta, na kwa kampuni nyingine, orodha ambayo Meta itakupa baada ya kupokea ombi lako lililoandikwa. Meta itafanya hivyo tu kwa kuwepo makubaliano yaliyoandikwa kati yake na Wachakataji-wengine kama hao, makubaliano ambayo yanaweka majukumu sawa ya ulindaji wa data kwa Wachakataji-wengine kama yalivyowekwa kwa Meta chini ya Makubaliano haya. Pale ambapo Mchakataji-mwingine huyo anaposhindwa kutimiza majukumu kama hayo, Meta itakuwa na wajibu kikamilifu kwa utendaji kukuhakikishia kwamba Mchakataji-mwingine anazingatia majukumu yake ya kulinda data.
    4. Pale ambapo Meta inahusisha Mchakataji mdogo au wa kuchukua nafasi ya mwingine, Meta itakujulisha kuhusu kuongeza au kubadilisha Mchakataji mwingine kama huyo katika muda usiopita siku kumi na nne (14) kabla ya kuajiriwa kwa mchakataji mdogo wa ziada au anayechukua nafasi ya mwenzake. Unaweza kukataa kuhusishwa kwa au kubadilishwa kwa Mchakataji-mwingine kama huyo katika muda wa siku kumi na nne (14) baada ya kuarifiwa na Meta kwa kusitisha Makubaliano haya mara moja kwa ilani ya maandishi ya Meta.
    5. Meta itakuarifu bila kuchelewa baada ya kujulishwa kuhusu Ukiukaji wa Data ya Kibinafsi unaohusiana na Data Yako ya Kibinafsi. Ilani kama hiyo itajumuisha, wakati wa taarifa au pindi tu baada ya taarifa, maelezo muhimu ya Ukiukaji wa Data ya Kibinafsi wanapopokea arifa au haraka iwezekanavyo baada ya kupokea ilani ikiwemo idadi ya rekodi zako zilizoathirika, kategoria na idadi ya Watumiaji walioathirika, madhara yanayotarajiwa ya ukiukaji huo na suluhu halisi au pendekezwa, panapofaa za kukabili athari zozote mbaya zinazoweza kutokana na ukiukaji huo.
    6. Kwa kiwango ambacho GDPR au sheria zozote za ulinzi wa data katika EEA, Uingereza au Uswizi zinatumika katika Uchakataji wa Data Yako chini ya Kiambatisho hiki cha Uchakataji wa Data, Kiambatisho cha Uhamishaji wa Data cha Ulaya inatumika kwa uhamishaji wa data unaofanywa na Meta Platforms Ireland Ltd na ni sehemu ya, na imejumuishwa kupitia marejeleo kwa Kiambatisho hiki cha Uchakataji wa Data.
  3. Masharti ya Mchakataji wa Marekani
    1. Kwa kadiri Masharti ya Mchakataji wa Marekani wa Meta yatatumika, yatakuwa sehemu ya, na yatajumuishwa kwa kurejelea katika Makubaliano haya, isipokuwa kwa Sehemu ya 3 (Majukumu ya Kampuni) ambayo haijajumuishwa wazi.









Kiambatisho cha Usalama wa Data

  1. Usuli na Lengo
    Waraka huu unafafanua mahitaji ya chini zaidi ya usalama yanayobana Meta katika kutoa kwake Workplace kwako.
  2. Mfumo wa Usimamizi wa Maelezo ya Usalama
    Meta imeunda na itadumisha Mfumo wa Usimamizi wa Maelezo ya Usalama (ISMS) ulioundwa ili kutekeleza matendo yanayozingatia vigezo vya kitaaluma vya usalama katika utaoji wake wa Workplace. Mfumo wa ISM wa Meta umeundwa kulinda dhidi ya ufikiaji bila idhini, utoaji, matumizi, kupotea au kubadilishwa kwa Data Yako.
  3. Mchakato wa Kudhibiti Hatari
    Usalama wa maelezo na wa rasilimali za uchakataji maelezo, ikiwemo miundo misingi ya Teknolojia ya Habari na rasilimali halisi, yatafanyiwa tathmini ya hatari. Tathmini ya hatari ya Workplace itafanywa kila mara.
  4. Upangaji wa Usalama wa Maelezo
    Meta imeweka afisa mteule wa Usalama aliye na wajibu wa kijumla wa kuhakikisha usalama kwenye shirika. Meta imeweka watu wateule ambao wajibu wao ni kuchunguza usalama wa huduma yako ya Workplace
  5. Usalama wa Eneo na Mazingira
    Hatua za kiusalama za Meta zitajumuisha vidhibiti vilivyosanifiwa ili kutoa hakikisho tosha kwamba ufikiaji rasilimali halisi ya uchakataji unakubaliwa tu kwa watu walioidhinishwa na kwamba vidhibiti vya mazingira vinawekwa kugundua, kuzuia na kudhibiti uharibifu unaotokana na uchafuzi wa mazingira. Vidhibiti hivyo ni pamoja na:
    Vidhibiti hivyo ni pamoja na:
    • Ufuatiliaji na ukaguzi wa ufikiaji wa moja kwa moja wa rasilimali uya uchakataji data na wafanyakazi na wanakandarasi;
    • Kuweka mifumo ya upelelezi ya kamera za siri zinazowekwa katika kila eneo la kuingia kwenye rasilimali ya uchakataji data;
    • Mifumo inayofuatalia na kudhibiti viwango vya joto a unyevu vya mitambo ya kompyuta; na
    • Nyenzo za umeme na jenereta.
    Meta itatekeleza taratibu zinazokubalika kitaaluma za kufuta data kwa njia salama kwenye maudhui ya kielektroniki, kulingana na Makubaliano.
  6. Kutenganishwa
    Meta itaunda taratibu za kiufundi za kuhakikisha kwamba Data Yako imetenganishwa kimantiki kutoka kwa data za wateja wengine na kwamba Data Yako inapatikana tu kwa watumiaji walioidhinishwa.
  7. Wafanyakazi
    1. Mafunzo
      Meta itahakikisha kwamba wafanyakazi wote wenye idhini ya kufikia Data Yako wanapata mafunzo kuhusu usalama.
    2. Ukaguzi na Uchunguzi wa Usuli
      Meta:
      • Itaweka mchakato wa kuthibitisha utambulisho wa wafanyakazi walio na huduma yako ya Workplace.
      • Itaweka mchakato wa kufanya ukaguzi kwa wafanyakazi wanaofanya kazi na huduma yako ya Workplace kulingana na vigezo vya Meta.
      Meta itawapa kadi za Utambulisho zilizo na picha na majina yaliyoandikwa kwa wafanyakazi wote wanaofanya kazi na huduma yako ya Workplace. Kadi za Utambulisho zitahitajika ili mtu aweze kuingia kwenye rasilimali zote za Meta.
    3. Ukiukaji wa Usalama wa Wafanyakazi
      Meta itaweka vikwazo dhidi ya wafanyakazi wake wanaojaribu kufikia Data Yako bila idhini ya Meta, ikiwa ni pamoja na, adhabu inayofikia na kujumuisha kutamatishwa.
  8. Majaribio ya Kiusalama
    Meta itafanya majaribio ya kila mara ya usalama na udhaifu ili kubaini ikiwa vidhibiti muhimu vinatekelezwa ipasavyo na vinafanya kazi.
  9. Udhibiti wa Ufikiaji
    1. Usimamizi wa Nenosiri la Mtumiaji
      itaweka mchakato thabiti wa Usimamiaji wa Nenosiri la Mtumiaji, uliosanifiwa kuhakikisha kwamba nenosiri linasalia kuwa ya kibinafsi na haiwezi kufikiwa na watu wasioidhinishwa, ikiwemo kwa kiwango cha chini zaidi:
      • Utoaji wa nenosiri, ukiwemo uthibithishaji wa utambulisho wa mtumiaji kabla ya nenosiri jipya, linalobadilishwa au la muda.
      • Kusimba manenosiri yote kwa njia fiche yanapohifadhiwa kwenye mifumo ya kompyuta au yanaposafirishwa mtandaoni.
      • Kubadilisha manenosiri yote chaguomsingi ya watoa huduma.
      • Manenosiri thabiti kulingana na matumizi yake lengwa.
      • Ufahamu kwa Watumiaji.
    2. Usimamizi wa Ufikiaji kwa Mtumiaji
      Meta itatekeleza mchakato kwa ajili ya kubadilisha na / au kubatilisha haki za ufikiaji na Vitambulisho vya Mtumiaji, bila kuchelewa bila sababu. Meta itaweka taratibu za kuripoti na kubatilisha hati tambulishi za ufikiaji zilizoathiriwa (nenosiri, tuzo n.k.) 24/7. Meta itatekeleza kumbukumbu zifaazo za usalama zikijumuisha kitambulisho cha mtumiaji na rekodi ya wakati. Saa italandanishwa na NTP.
      Matukio yafuatayo ya kiwango cha chini zaidi yatarekodiwa:
      • Mabadiliko kwenye Idhini;
      • Uthibitishaji wa majaribio yaliyofaulu na yaliyokosa kufaulu; na
      • Utendakazi wa kusoma na kuandika.
  10. Usalama wa Mawasiliano
    1. Usalama wa Mtandao
      Meta itatumia teknolojia inayoambatana na vigezo vya kitaaluma vya kutenganisha mtandao.
      Ufikiaji wa mtandao wa mbali utahitaji mawasiliano yaliyosimbwa kwa njia fiche kwa kutumia itifaki salama na kutumia uhalalishaji wa vipengee anuwai.
    2. Ulindaji wa Data unaosafirishwa
      Meta itatekeleza matumizi ya itifaki ifaayo iliyosanifiwa kulinda siri ya data inayosafirishwa kwenye mitandao.
  11. Usalama wa Operesheni
    Meta itaratibu na kudumisha mpango wa kudhibiti udhaifu kwa ajili ya Workplace ambayo inajumuisha ufafanuzi wa majukumu na wajibu, umiliki wa ufuatiliaji wa udhaifu, tathmini ya hatari ya udhaifu na utoaji wa nyenzo za kiusalama wa mtandao.
  12. Udhibiti wa Tukio la Usalama
    Meta itaunda na kudumisha mpango kushughulikia tukio la usalama kwa ajili ya kufuatilia, kugundua na kushughulikia matukio yanayoweza kutokea ya usalama yanayoathiri huduma yako ya Workplace. Mpango huo wa kushughulikia tukio la usalama utajumuisha angalau ufafanuzi wa majukumu na wajibu, mawasiliano na ukaguzi wa tathmini za baadaye, ikiwa pamoja na uchanganuzi wa kina wa sababu na mipango ya kusuluhisha.
    Meta itafuatilia Workplace ili kugundua ukiukaji wowote wa usalama na shughuli za uhadaaji. Mchakato wa ufuatiliaji na mbinu za ugunduaji zitasanifiwa ili kuruhusu ugunduaji wa matukio ya usalama yanayoathiri huduma yako ya Workplace kulingana na hatari zifaazo na utambuzi unaoendelea wa hatari.
  13. Uendelevu wa Biashara
    Meta itadumisha mpango wa uendelevu wa biashara ya kushughulikia masuala ibuka au hali nyingine muhimu yanayoweza kuharibu huduma yako ya Workplace. Meta itakagua mpango wa uendelevu wa biashara kirasmi angalau mara moja kila mwaka.
Ilisasishwa mwisho: Machi 27 2023