Sera ya Vidakuzi vya Workplace


Sera hii ya Vidakuzi vya Workplace (“Sera ya Vidakuzi”) inafafanua jinsi tunavyotumia vidakuzi na inapaswa kusomwa pamoja na Sera ya Faragha ya Workplace ambayo itatumika kuchakata data yetu ya kibinafsi tunayokusanya kupitia vidakuzi. Sera hii ya Vidakuzi haitumiki unapotembelea tovuti ya uuzaji na maelezo ya umma workplace.com (“Tovuti ya Workplace”).
Vidakuzi na Teknolojia Nyingine za Hifadhi
Vidakuzi ni matini madogo yanayotumiwa kuhifadhi maelezo kwenye vivinjari vya wavuti. Vidakuzi vinatumiwa kuhifadhi na kupokea vitambulishi na maelezo mengine kwenye kompyuta, simu, na vifaa vingine. Teknolojia zingine, pamoja na data tunayohifadhi kwenye kivinjari chako cha wavuti au kifaa, vitambuzi vinavyohusiana na kifaa chako, na programu nyingine, hutumiwa kwa malengo sawa. Katika sera hii, tunarejelea teknolojia hizi zote kama “vidakuzi”.
Tunatumia vidakuzi wapi?
Tunaweza kuweka vidakuzi kwenye kompyuta au kifaa chako, na kupokea maelezo yaliyohifadhiwa katika vidakuzi, unapotumia bidhaa ya mtandaoni ya Workplace ambayo tunatoa kwa wateja wetu (shirika ambalo unafanyia kazi au ambalo lilitoa akaunti yako) ambayo huruhusu watumiaji kushirikiana na kushiriki maelezo kazini, ikijumuisha bidhaa ya Workplace, programu na huduma husika za mtandaoni (kwa pamoja “Huduma za Workplace”).
Vidakuzi hudumu kwa muda gani?
Vidakuzi vyote vina tarehe za mwisho wa matumizi ambazo hubainisha muda wa kukaa kwenye kivinjari chako au kwenye kifaa chako na hivi vinaweza kugawanywa katika vikundi viwili:
  • Vidakuzi vya Kipindi – hivi ni vidakuzi vya muda ambavyo huisha muda wake (na hufutwa kiotomatiki) kila wakati unapofunga kivinjari chako.
  • Vidakuzi vya Kujirudia – kwa kawaida huwa na tarehe ya mwisho wa matumizi na kwa hivyo hubaki kwenye kivinjari chako hadi muda wake wa matumizi kuisha, au hadi uvifute wewe mwenyewe.
Mbona tunatumia vidakuzi?
Vidakuzi hutusaidia kutoa, kulinda na kuboresha Huduma za Workplace, kama vile kubinafsisha maudhui na kutoa uzoefu salama.
Hasa, tunazitumia kwa madhumuni yafuatayo:
Aina ya KidakuziLengo
Uhalalishaji
Tunatumia vidakuzi kuthibitisha akaunti yako na kutambua unapokuwa umeingia katika akaunti ili tuweze kukusaidia kufikia Huduma za Workplace kwa urahisi na kukuonyesha matumizi na vipengele vinavyofaa.
Kwa mfano: Tunatumia vidakuzi pia kutusaidia kukumbuka kivinjari chako ili usilazimike kuendelea kuingia katika Huduma za Workplace.
Usalama, tovuti na uadilifu wa bidhaa
Tunatumia vidakuzi kutusaidia kudumisha usalama wa akaunti, data na Huduma zako za Workplace salama.
Kwa mfano: Vidakuzi vinaweza kutusaidia kutambua na kuweka hatua za ziada za usalama endapo mtu anajaribu kufikia akaunti ya Workplace bila idhini, kwa mfano, kwa kujaribu kutabiri nenosiri tofauti mara kadhaa. Kadhalika, tunatumia vidakuzi ili kuhifadhi maelezo yanayoturuhusu kurejesha akaunti yako endapo utasahau nenosiri lako au ukihitaji uhalalishaji wa ziada ukituambia akaunti yako imelaghaiwa.
Pia tunatumia vidakuzi kupambana na shughuli zinazokiuka sera zetu au vinginevyo zinashusha hadhi ya uwezo wetu wa kutoa Huduma za Workplace.
Vipengele na huduma
Tunatumia vidakuzi kutoa vipengele vinavyotusaidia kutoa Huduma za Workplace.
Kwa mfano: Vidakuzi hutusaidia kuhifadhi mapendeleo, kujua wakati umeona au kuingiliana na maudhui ya Workplace, na provCookies hutusaidia kuhifadhi mapendeleo, kujua wakati umeona au kuingiliana na maudhui ya Workplace, na kukupa maudhui na matumizi yaliyobinafsishwa. Pia tunatumia vidakuzi ili kusaidia kukutolea maudhui muhimu kwa eneo lako.
Kwa mfano: Tunahifadhi maelezo kwenye kidakuzi kinachowekwa kwenye kivinjari au kifaa chako ili uweze kuona huduma katika lugha uliyochagua.
Utendakazi
Tunatumia vidakuzi ili kukutolea hali nzuri ya matumizi iwezekanavyo.
Kwa mfano: Vidakuzi hutusaidia kupanga trafiki kati ya seva na kuelewa Huduma za Workplace hupakiwa haraka kiasi gani kwa watu tofauti. Vidakuzi pia hutusaidia kurekodi vipimo na ukubwa wa skrini na madirisha yako na kujua ikiwa umewasha hali ya juu ya ubainifu ili tuweze kuwasilisha tovuti na programu zetu ipasavyo.
Uchanganuzi na utafiti
Tunatumia vidakuzi ili kuelewa vyema jinsi watu hutumia Huduma za Workplace ili tuweze kuziimarisha.
Kwa mfano: Vidakuzi vinaweza kusaidia kuelewa jinsi watu hutumia Huduma za Workplace, kuchanganua sehemu zipi za Huduma za Workplace ambazo zinawafaidi sana watu na kuhusisha na kutambua vipengele vinavyoweza kuboreshwa.
Tunatumia vidakuzi gani?
Vidakuzi ambavyo tunamia vinajumuisha vidakuzi vya kipindi, vinavyofutwa unapofunga kivinjari chako, na vidakuzi vya kila mara, vinavyokaa kwenye kivinjari chako hadi viishe muda au uvifute.
Tunaweka vidakuzi vya wahusika wa kwanza pekee katika Huduma za Workplace. Vidakuzi vya mhusika mwingine havijawekwa katika Huduma za Workplace
Unawezaje kudhibiti matumizi yetu ya vidakuzi?
Kivinjari au kifaa chako kinaweza kutoa mipangilio inayokuruhusu kuchagua iwapo vidakuzi vya kivinjari vimewekwa na kuvifuta. Kwa maelezo zaidi kuhusu vidhibiti hivi, tembelea nyenzo za msaada za kivinjari au kifaa chako. Huenda sehemu fulani ya Huduma za Workplace ikakosa kufanya kazi ipasavyo ikiwa umelemaza matumizi ya vidakuzi kwenye kivinjari.

Tarehe ya marekebisho ya mwisho: Juni 10 2022