MAKUBALIANO YA BILI

KWA KUBOFYA UNAKUBALI MAKUBALIANO HAYA YA BILI, UNADHAMINI NA KUWAKILISHA KWAMBA UNAINGIA KATIKA MAKUBALIANO HAYA YA BILI KWA NIABA YA KAMPUNI AU SHIRIKA LINGINE KISHERIA NA KWAMBA UNA IDHINI KAMILIFU YA KUFUMBATA SHIRIKA KAMA HILO KWENYE MAKUBALIANO HAYA YA BILI. KUREJELEWA KWA “WEWE”, “YAKO” AU “MTEJA” KUNA MAANA YA SHIRIKA KAMA HILO.
Ikiwa eneo lako msingi la biashara lipo Marekani au Kanada, Makubaliano haya ya Bili ni makubaliano kati yako na Meta Platforms, Inc. Vinginevyo, Makubaliano haya ya Bili ni makubaliano kati yako na kampuni ya Meta Platforms Ireland Ltd. Kurejelewa kwa “Meta”, “nasi”, “sisi”, au “yetu” kuna maana ya Meta Platforms, Inc. au Meta Platforms Ireland Ltd, kama inavyofaa.
Makubaliano haya ya Bili yanahusu makubaliano yako yaliyopo na Meta kwa ajili ya matumizi ya Workplace kutoka kwa huduma ya Meta ("Makubaliano"). Masharti yenye herufi kubwa katika Makubaliano haya ya Bili yana maana yaliyopewa katika Makubaliano, isipokuwa kama yameelezwa vinginevyo.
Masharti ya Makubaliano haya ya Bili yanajumuishwa kwa kurejelea katika Makubaliano yako. Iwapo yatakinzana na masharti yoyote ya Makubaliano yako ya sasa kabla ya Makubaliano haya ya Bili kuanza kutumika, basi masharti ya Makubaliano haya ya Bili yatachukua nafasi ya kwanza. Ikiwa kwa sasa huna makubaliano ya kutumia Workplace, basi Masharti yafuatayo ya Mtandaoni ya Workplace yatatumika kwa matumizi yako ya Workplace na yametumika tangu ulipoanza kutumia.
1. Ada. Masharti yote kuhusu ada, masharti ya malipo na ushuru yanayohusiana na matumizi yako ya Workplace yatakuwa kama yalivyobainishwa katika Masharti ya Workplace ya Mtandaoni, isipokuwa kama itakubaliwa vinginevyo.
2. Masharti ya Ziada ya Malipo ya Kadi ya Mkopo.
a. Mamlaka. Unapotupea kifaa chako cha malipo, unathibitisha kuwa unakibali cha kutumia kifaa hicho cha kufanyia malipo. Unapogharamia muamala, unatuidhinisha (pamoja na wachakata malipo wengine maalum) kutoza kiasi kizima kwenye kifaa cha kufanyia malipo ambacho unataka kukifanyia muamala. Pia unatuidhinisha kukusanya na kuhifadhi maelezo ya muamala. Ikiwa una eneo lako kuu la biashara nchini Marekani au Kanada, basi unaidhinisha Facebook Payments Inc., ambayo ni kampuni ya Florida, kuhifadhi kifaa chako cha kufanyia malipo. Ili uone Sera ya Faragha ya kampuni ya Facebook Payments Inc, tafadhali tembelea: https://www.facebook.com/payments_terms/privacy. Ikiwa una eneo lako kuu la biashara katika nchi nyingine kando na Marekani au Kanada, basi unaidhinisha Facebook Payments International Ltd., ambayo ni kampuni ya kibinafsi iliyo katika Jamhuri ya Ayalandi, kuhifadhi kifaa chako cha kufanyia malipo.
b. Uidhinishaji. Iwapo utalipa ukitumia kadi ya mkopo au ya malipo, tunaweza kupata uidhinishaji awali kutoka kwa mtoaji wa kadi kwa kiwango ambacho kinaweza kuwa juu sawa na kiwango kamili cha ununuzi wako. Tutatoza kadi yako wakati unapoanzisha malipo au muda mfupi baadaye. Iwapo utakatisha muamala kabla ya kukamilika, uidhinishaji awali unaweza kusababisha pesa hizo kutopatikana kwako mara moja.
c. Malipo ambayo hayakufaulu. Iwapo muamala wa malipo yako utasababisha mkopo au ada nyingine kutoka kwa benki yako, wewe pekee ndiye utawajibikia ada hiyo.
d. Haki yetu ya kukatisha. Tunaweza kukatisha muamala wowote ikiwa tunaamini kuwa muamala huo unakiuka Makubaliano haya au ikiwa tunaamini kufanya hivyo kunaweza kuzuia hasara ya kifedha.
e. Vikwazo vya malipo, Ili kukuepusha wewe pamoja na sisi kupoteza pesa, tunaweza kuchelewesha malipo kwa muda fulani, au kuwekea kifaa chako cha kufanyia malipo viwango vya kufanya muamala, au kukuwekea viwango vya ununuzi unaoweza kufanya au kufunga akaunti yako.
f. Kushiriki maelezo. Ili kukuepusha wewe pamoja na sisi kupoteza pesa, tunaweza kuwasiliana na mtoa kifaa chako cha kufanyia malipo, watekelezaji wa sheria au wahusika wengine wanaoathirika (wakiwemo watumiaji wengine) na kushiriki maelezo kuhusu malipo unayohusishwa nayo, ikiwa tutaamini kuwa kwa kufanya hivyo tutakuwa tumezuia kupoteza pesa au ukiukaji wa sheria.
g. Usalama. Utawajibika kwa kudumisha usalama wa akaunti yako ya Workplace na unaelewa kuwa utagharamia maagizo yoyote yatakayofanywa kwenye au kupitia akaunti yako.
h. Ukatishaji. Malipo yanayojirudia yataghairiwa baada ya Makubaliano haya kuhitimishwa, mradi tu pesa zote zinazodaiwa zimelipwa kikamilifu.
i. Akaunti za wahalifu. Ikiwa njia yako ya malipo itashindwa au akaunti yako ipite makataa, tunaweza kuchukua hatua za kukusanya kiasi cha pesa ambazo hukulipa kwa kutumia mbinu nyinginezo za kukusanya. Unakubali kulipa gharama zote zinazohusiana na kuokoa pesa huko ikiwa ni pamoja na ada tumika za kisheria.