Kiambatisho cha Uchakataji wa Data

  1. Ufafanuzi
    Ndani ya Kiambatisho hiki cha Uchakataji Data, “GDPR” ina maana ya Kanuni ya Kawaida ya Ulindaji Data (Kanuni ya (EU) 2016/679), na maneno haya “Mdhibiti”, “Mchakataji Data”, “Mhusika wa Data”, “Data ya Kibinafsi”, “Ukiukaji wa Data Binafsi” na “Uchakataji” yatakuwa na maana sawa kama yalivyofafanuliwa katika GDPR. “Imechakatwa” na “Chakata” yataeleweka kulingana na ufafanuzi kuhusu maana ya “Uchakataji”. Marejeleo ya GDPR na utoleaji wake yanajumuisha GDPR ilivyorekebishwa na kuingizwa kwenye sharia ya Uingereza. Istilahi nyingine zote zilizofafanuliwa hapa zitakuwa na maana sawa kama zilivyofafanuliwa kwingineko kwenye Makubaliano haya.
  2. Uchakataji wa Data
    1. Kwa kutekeleza shughuli zake kama Mchakataji chini ya Makubaliano haya kuhusiana na Data yoyote ya Kibinafsi kwenye Data Yako (“Data Yako ya Kibinafsi”), Meta inathibitisha kwamba:
      1. kipindi, mada, hali na madhumuni ya Uchakataji huu yatabainishwa kwenye Makubaliano haya;
      2. aina za Data ya Kibinafsi Zinazochakatwa zitajumuisha zile zilizobainishwa kwenye ufafanuzi wa Data Yako;
      3. kategoria za Wamiliki wa Data zinajumuisha wawakilishi wako, Watumiaji na watu wengine waliotambuliwa au wanaweza kutambulika kupitia Data Yako ya Kibinafsi; na
      4. majukumu na haki zako kama Mdhibiti Data kuhusiana na Data yako ya Kibinafsi zimeelezwa kwenye Makubaliano haya.
    2. Kwa kiwango ambacho Meta Huchakata Data yako ya Kibinafsi chini ya au kuhusiana na Makubaliano, Meta:
      1. itachakata tu Data yako ya Kibinafsi kulingana na maelezo yako kama yalivyoelezwa kwenye Makubaliano haya, ikiwa ni pamoja na kwa mujibu wa uhamishaji wa Data yako ya Kibinafsi, kwa kutegemea hali za kipekee zilizoruhusiwa chini ya Kifungu cha 28(3)(a) cha GDPR;
      2. itahakikisha kwamba wafanyakazi wake walio na idhini ya Kuchakata Data Yako ya Kibinafsi chini ya Makubaliano haya wameapa kuzingatia siri au wanadhibitiwa na sheria kuhusu majukumu ya kulinda siri kuhusiana na Data yako ya Kibinafsi;
      3. itatekeleza hatua za kiufundi na za kishirika zilizobainishwa kwenye Kiambatisho cha Usalama wa Data;
      4. itazingatia kanuni zinazorejelewa hapa chini kwenye Sehemu ya 2.c na 2.d ya Kiambatisho cha Uchakataji Data inapowateua Wachakataji- wa kiwango cha chini;
      5. itakusaidia kwa kukupa hatua zifaazo za kiufundi na za kishirika kadri hii inavyowezekana kupitia Workplace, ili kukuwezesha kutimiza wajibu wako wa kujibu maombi ya Mmiliki Data ya kutekeleza haki chini ya Sura ya III ya GDPR;
      6. itakusaidia kuhakikisha unazingatia majukumu yako kwa mujibu wa Kifungu cha 32 hadi 36 ya GDPR kwa kuzingatia hali ya Uchakataji na maelezo yanayotolewa kwa Meta;
      7. endapo Makubaliano yatasitishwa, Facebook, itafuta Data ya Kibinafsi kwa mujibu wa Mkataba isipokuwa endapo Umoja wa Ulaya au sheria za nchi mwanachama zitahitaji kwamba Data ya Kibinafsi ihifadhiwe;
      8. itakupa maelezo yote yaliyoelezwa kwenye Makubaliano haya na kupitia Workplace katika kutimiza majukumu ya Meta ya kutoa maelezo yote muhimu ili kuonyesha Meta inatii majukumu yake chini ya Kifungu cha 28 cha GDPR; na
      9. baada ya kila mwaka, Meta inakubali kwamba itachagua kampuni nyingine itakayoendesha shughuli ya ukaguzi ya SOC 2 Aina ya II au ukaguzi mwingine unaokubalika kitaaluma wa udhibiti wa Meta kuhusiana na Workplace, unazipa uwezo kikazi kampuni nyingine kama hizo. Ikiwa utaomba, Meta itakupa nakala ya ripoti ya ukaguzi ya wakati huo na ripoti kama hiyo itazingatiwa kuwa ni Maelezo ya Siri ya Meta.
    3. Unaidhinisha Meta kuwapa kandarasi ya majukumu ya Uchakataji data chini ya Makubaliano haya kwa Washirika wa Meta, na kwa kampuni nyingine, orodha ambayo Meta itakupa baada ya kupokea ombi lako lililoandikwa. Meta itafanya hivyo tu kwa kuwepo makubaliano yaliyoandikwa kati yake na Wachakataji-wengine kama hao, makubaliano ambayo yanaweka majukumu sawa ya ulindaji wa data kwa Wachakataji-wengine kama yalivyowekwa kwa Meta chini ya Makubaliano haya. Pale ambapo Mchakataji-mwingine huyo anaposhindwa kutimiza majukumu kama hayo, Meta itakuwa na wajibu kikamilifu kwa utendaji kukuhakikishia kwamba Mchakataji-mwingine anazingatia majukumu yake ya kulinda data.
    4. Pale ambapo Meta inahusisha au kubadilisha Mchakataji-mwingine kuanzia (i) 25 Mei 2018, au (ii) Tarehe ya Kuanza kutumika (Tarehe yoyote ile itakuja baadaye), Meta itakuarifu kuhusu kuongezwa huko au kubadilishwa kwa Wachakataji-wengine katika muda usiozidi siku kumi na nne (14) kabla ya kuteuliwa kwa au kubadilishwa kwa Mchakataji-mwingine kama huyo. Unaweza kukataa kuhusishwa kwa au kubadilishwa kwa Mchakataji-mwingine kama huyo katika muda wa siku kumi na nne (14) baada ya kuarifiwa na Meta kwa kusitisha Makubaliano haya mara moja kwa ilani ya maandishi ya Meta.
    5. Meta itakuarifu bila kuchelewa baada ya kujulishwa kuhusu Ukiukaji wa Data ya Kibinafsi unaohusiana na Data Yako ya Kibinafsi. Ilani kama hiyo itajumuisha, wakati wa taarifa au pindi tu baada ya taarifa, maelezo muhimu ya Ukiukaji wa Data ya Kibinafsi wanapopokea arifa au haraka iwezekanavyo baada ya kupokea ilani ikiwemo idadi ya rekodi zako zilizoathirika, kategoria na idadi ya Watumiaji walioathirika, madhara yanayotarajiwa ya ukiukaji huo na suluhu halisi au pendekezwa, panapofaa za kukabili athari zozote mbaya zinazoweza kutokana na ukiukaji huo.
    6. Kwa kiwango ambacho GDPR au sheria zozote za ulinzi wa data katika EEA, Uingereza au Uswizi zinatumika katika Uchakataji wa Data Yako chini ya Kiambatisho hiki cha Uchakataji wa Data, Kiambatisho cha Uhamishaji wa Data cha Ulaya inatumika kwa uhamishaji wa data unaofanywa na Meta Platforms Ireland Ltd na ni sehemu ya, na imejumuishwa kupitia marejeleo kwa Kiambatisho hiki cha Uchakataji wa Data.
  3. Masharti ya Mchakataji wa Marekani
    1. Kwa kadiri Masharti ya Mchakataji wa Marekani wa Meta yatatumika, yatakuwa sehemu ya, na yatajumuishwa kwa kurejelea katika Makubaliano haya, isipokuwa kwa Sehemu ya 3 (Majukumu ya Kampuni) ambayo haijajumuishwa wazi.