Sera ya Faragha ya Workplace Standard

Workplace Standard huruhusu watumiaji walio katika shirika au eneo moja la kazi (“Biashara”) au jamii zao kushirikiana, kushiriki na kugundua maelezo ya kazi kwa njia bora zaidi. Sera hii ya Faragha inafafanua jinsi na wakati gani maelezo yako hukusanywa, kutumiwa na kushirikiwa na Facebook wakati wewe, wafanyakazi wenzako, washirika wa kibiashara au watumiaji wengine wanapotumia jukwaa la Workplace Standard (ambayo ni pamoja na tovuti, programu na huduma sawia za mtandaoni za Workplace ambazo huunganishwa kwenye Sera hii ya Faragha, ambayo tunaita “Huduma”) Sera Hii ya Faragha hutumika katika utumiaji wako wa Huduma. Huduma nyingine za Facebook hudhibitiwa na masharti yazo binafsi.
ILANI MUHIMU: Tunazipa biashara chaguo za Workplace Essential, Workplace Advance au Workplace Enterprise, zinazoruhusu Biashara kuchukua udhibiti wa akaunti zote za Workplace Standard ambazo Biashara inaweza kuonyesha umiliki wa kikoa cha anwani ya barua pepe (“Akaunti Zilizoboreshwa”) na kuboresha akaunti hizi ziwe jumuiya mpya ya Workplace Essential, Workplace Advanced au Workplace Enterprise. Hii huipa Biashara uwezo wa kufikia, kuchakata na kufuta data yoyote iliyotumwa au uliyotolewa hapo awali kupitia kwenye Huduma na Watumiaji Walioboresha, ikiwemo faili na mawasiliano yote, ujumbe wa Gumzo kwenye makundi yote na Workplace.
Iwapo umejiunga kwenye Workplace Standard ukitumia anwani ya barua pepe, nambari ya simu au maelezo mengine ambayo hayamilikiwa na Biashara, lakini umeshiriki maudhui ndani ya jumuiya ya Biashara (ikiwa ni pamoja na data zote zilizoshirikiwa katika vikundi ndani ya jumuiya ya Biashara na katika Gumzo ya Workplace na Watumiaji Walioboresha), basi Biashara baada ya kuboresha ii itumie jumuiya ya Workplace Essential, Workplace Advance au Workplace Enterprise, itaweza kufikia na kudhibiti data zote zilizowasilishwa au kutolewa kupitia Huduma ndani ya kikundi au jumuiya ya Biashara hiyo. Hii itakuwa ni pamoja na faili na mawasiliano yote ambayo yalishirikiwa hapo awali na yale yanaweza kushirikiwa siku zijazo kupitia Akaunti Zilizoboreshwa katika kikundi hicho cha Biashara au jumuiya, ikiwa ni pamoja na Gumzo la Workplace kwa Watumiaji Walioboresha Akaunti.
Ikiwa Biashara itachagua kuboresha ili itumie Workplace Essential, Workplace Advanced au Workplace Enterprise, basi huenda ukalazimika kukubali seti mpya ya masharti wakati huo, ikiwa ni pamoja na sera mpya ya faragha na masharti ya matumizi. Kwa maelezo zaidi kuhusu tofauti kati ya Workplace Standard, Workplace Essential, Workplace Advanced na Workplace Enterprise au kuboresha akaunti yako tazama hapa. Ikiwa Biashara itateua kuboresha ili itumie Workplace Essential, Workplace Advanced au Workplace Enterprise, itakuwa Biashara hiyo wala sio Facebook itakayobainisha jinsi maelezo yako yanaweza kuchakatwa na kutumika katika jumuiya hiyo ya Biashara ya Workplace, ikiwa ni pamoja na maelezo ambayo awali ulishiriki kwenye Workplace Standard ndani ya kikundi au jumuiya hiyo ya Biashara.
Tafadhali hakikisha kwamba unavyo vibali na idhini zote zinazohitajika kabla ya kuchapisha maelezo yoyote kuhusu watumiaji wengine wa Huduma hizi au Biashara yako kwenye jukwaa la Workplace.

I. Je, tunakusanya maelezo ya aina gani?
Maelezo ambayo wewe na wengine hutoa. Tunaweza kukusanya aina zifuatazo za maelezo kutoka kwako na yanayokuhusu:
 • Maudhui na maelezo mengine unayotoa unapotumia Huduma zetu, ikiwa ni pamoja na unapojisajili kwenye akaunti, kuunda au kushiriki na kuwasiliana au kuwatumia wenzako ujumbe. Hii inaweza kujumuisha maelezo ya au kuhusu maudhi unaotoa, kama vile tarehe ambapo faili fulani iliundwa. Pia tunakusanya maelezo kuhusu jinsi unavyotumia Huduma zetu, kama vile aina za maudhui unayotazama au kutagusana nayo au mara na kipindi unachokichukua katika shughuli zako;
 • maelezo ya anwani, kama vile jina kamili na anwani ya barua pepe na maelezo yoyote ya anwani za watumiaji wengine (kama vile nambari zao za simu au anwani za barua pepe) ambayo unachagua kupakia, kulandanisha au kuhamisha (kama vile kutoka katika Akaunti yako Binafsi ya Facebook);
 • cheo kazini, maelezo ya idara, miundo ya kuripoti na maelezo mengine yanayohusiana na kazi yako au Biashara;
 • mawasiliano na maelezo ambayo watu wengine hutoa wanapotumia Huduma. Hii inaweza kuwa maelezo kukuhusu kama vile watu wengine wanaposhiriki au kutoa maoni kwenye picha yako, kukutumia ujumbe au kupakia, kusawazisha au kuhamisha maelezo ya anwani yako;
 • maudhui kuhusu mawasiliano yote kwenye au kupitia kwenye Huduma;
 • mawasiliano ya mtumiaji, maoni, mapendekezo na mawazo yanayotumwa kwetu au maelezo mengine ambayo unatupa wakati wewe au Biashara yako inapowasiliana au kutuhusisha katika kutafuta usaidizi unaohusiana na Huduma;
 • maelezo kuhusu watu na makundi ambayo umeunganishwa nayo na jinsi unavyotagusana nao, kama vile watu unaowasiliana nao sana au makundi unayopenda kushirikiana sana; na
 • maelezo mengine yoyote unayochagua kupakia, kushiriki na watu wengine au kutoa kwetu moja kwa moja kupitia Huduma.
Maelezo tunayokusanya kutoka kwa familia ya kampuni za Facebook na kutoka kwenye Huduma za Facebook.
Tunaweza kupokea maelezo kukuhusu kutoka katika Huduma nyingine za Facebook unayochagua kutumia, kama vile akaunti yako Binafsi ya Facebook na kutoka kwa kampuni nyingine zinazomilikiwa au kuendeshwa na Facebook, kwa mujibu wa masharti na sera zao za faragha. Tunaweza kutumia maelezo haya kwa madhumuni yaliyoelezwa katika sehemu ya “Tunatumia maelezo haya vipi?” ya Sera ya Faragha. Pata maelezo zaidi kuhusu kampuni hizi za Facebook na sera zao za faragha, pamoja na Sera ya Data ya Facebook.
Maelezo kutoka washirika wa kampuni nyingine. Tunaweza pia kupokea maelezo kutoka kwa kampuni nyingine washirika wetu kukuhusu na shughuli zako kwenye na nje ya Workplace, kama vile maelezo kutoka kwa washirika wetu tunaposhirikiana kukupa huduma.
Maelezo kuhusu kifaa/eneo.Tunaweza kukusanya maelezo kutoka kwa au kuhusu kompyuta, simu au vifaa vingine ambapo unasakinisha na kufikia Huduma zetu, yakiwemo wala sio tu maelezo kuhusu maeneo (ikijumuisha maeneo mahususi ya kijiografia), kama vile kupitia kwenye GPS, Bluetooth au kupitia ishara za WiFi. Tunaweza kuhusisha au kuunganisha maelezo tunayokusanya kutoka kwenye vifaa vyako tofauti yanayotusaidia kukupa Huduma thabiti kwenye vifaa vyako mbalimbali.
Kumbukumbu na data ya vidakuzi. Tunakusanya kiotomatiki maelezo fulani yanayotolewa na kivinjari chako au mfumo wako wa kuendesha kupitia kwenye Huduma, kama vile anwani yako ya IP na vitambuzi vingine vya kivinjari au kifaa, aina ya kivinjari, mfumo wa uendeshaji, data ya mtandao kukataa kufanya kazi, Mtoa huduma ya Intaneti, ukurasa unaotembelea kabla na baada ya kutumia Huduma, tarehe na saa ulipoutembelea, maelezo kuhusu shughuli zako na hatua (kama vile viungo unavyobofya na ukurasa unaotazama) kwenye Huduma na maelezo ya kumbukumbu kwenye seva nyingine za kawaida (“Data ya Kumbukumbu na Kidakuzi”).
Tunaweza kuweka au kufanya data inayohifadhiwa kwenye vidakuzi au vifaa vya kawaida vya kuhifadhi kukusanya maelezo kiotomatiki. Unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu matumizi yetu ya vidakuzi na teknolojia zinazohusiana, ikiwa ni pamoja na madhumuni yetu ya kuyatumia kwa kusoma Sera yetu kuhusu Kidakuzi. Kwa kutumia Huduma hizi, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi na teknolojia sawia kama ilivyoelezwa kwenye Sera yetu ya Faragha.
Huenda kivinjari au kifaa chako kikatoa mipagilio inayohusiana na teknolojia hizi. Kwa maelezo zaidi kuhusu ikiwa maelezo haya yanapatikana, matumizi yake na jinsi yanafanya kazi, tembelea mwongozo wa usaidizi wa kivinjari au kifaa chako. Tunaweza kutambua au kujibu mawimbi kuhusu ufuatiliaji wa kivinjari au kifaa na mipangilio mingine inaweza kutatiza matumizi yako ya vipengele tunavyotoa. Pia, mipangilio inayotolewa na kivinjari au kifaa kila mara hutekelezwa tu kwa kivinjari au kifaa hicho.

II. Je, tunatumiaje maelezo tunayoyakusanya?
Facebook itatumia maelezo tunayokusanya kutoa, kuunda, kuboresha na kufanya Huduma hizi kuwa na thamani kifedha, pamoja na Huduma za Facebook na zile huduma zinatolewa na Kampuni za Facebook. Mifano ya hayo ni pamoja na:
 • Kuwasiliana na watumiaji kuhusiana na matumizi yao ya Huduma;
 • Kuimarisha na kuendeleza usalama na uadilifu wa Huduma kwako na watumiaji wengine;
 • Kuendesha, kudumisha na kuboresha mifumo na miundo-msingi inayotoa Huduma na Huduma nyingine za Facebook (kumbuka kwamba tunatumia mifumo na miundo misingi sawa kusaidia Huduma hizi na Huduma za Facebook). Kwa mfano, tunaweza kutumia kumbukumbu za tovuti kukataa kufanya kazi kutoka kwenye matumizi yako ya Huduma ili kutambua na kurekebisha hitilafu zinazoweza kuwepo kwenye Huduma za Facebook;
 • kubinafsisha na kuweka mapendeleo ya matumizi yako kama sehemu ya utoaji wetu wa Huduma pamoja na kukupa maudhui, mawasiliano au mada (yakiwemo maudhui yaliyolipiwa) ambayo unaweza kuvutiwa nayo au yaliyo maarufu au yanayovuma kwenye jumuiya ya Biashara yako;
 • kuunda zana mpya, bidhaa na huduma tunazoweza kuleta ambazo zinaweza kuunda na kukupa matumizi bora zaidi kila wakati;
 • kutuma mawasiliano yako ya kutafutia bidhaa soko, kuwasiliana nawe kuhusu Huduma zetu na kukuruhusu ujue kuhusu sera na masharti yetu. Pia tunatumia maelezo yako kukujibu unapowasiliana nasi;
 • kuhusisha shughuli kwenye Huduma zetu na Huduma za Facebook kwenye vifaa mbalimbali zinazoendeshwa ua kutumiwa na mtu sawa kuboresha Huduma na Huduma nyingine za Facebook tunazotoa; na
 • kuendesha uchanganuzi wa data na mfumo, ikiwa ni pamoja na utafiti wa kuboresha Huduma na Huduma za Facebook.

III. Maelezo haya hushirikiwa vipi?
Tunaweza kushiriki maelezo tunayokusanya katika hali zifuatazo:
 • kwa jumuiya unapochagua kushiriki na kuwasiliana kupitia Huduma hii. Unaweza kuchagua hadhira unayochagua kushiriki nao maudhui nao, kwa mfano unaposhiriki maudhui kwenye Kikundi au unapotumia Gumzo la Workplace;
 • kwa Biashara katika hali ambapo Biashara inachukua udhibiti wa jumuiya ya Workplace, kama ilivyoelezwa hapa juu na kwenye Masharti ya Huduma ya Workplace Standard. Katika hali kama hizo, Biashara hiyo itakuwa inawajibikia namna maelezo yako yanavyotumiwa;
 • kwa watoa huduma kutoka kampuni nyingine ambao wanaweza kusaidia katika kutoa Huduma au sehemu ya Huduma;
 • kwa Kampuni za Facebook kwa madhumuni yaliyoelezwa hapa juu;
 • kwa programu tovuti au huduma nyingine unayoweza kuunganishwa nayo kupitia kwenye Huduma;
 • kuhusiana na mchakato muhimu wa kibiashara, kama vile uhamishaji wa Huduma, kuungana kwa kampuni, kuimarisha, uuzaji wa mali au katika tukio lisilotarajiwa la kufilisika au kutokuwa na pesa au ikiwa umiliki au udhibiti wa Huduma zetu zote au sehemu yake au mabadiliko ya mali, tunaweza kuhamisha maelezo yako kwa mmiliki mpya;
 • ili kusaidia kuthibitisha akaunti na shughuli na kuhimiza usalama ndani na nje ya Huduma na Huduma za Facebook, kama vile kuchunguza shughuli za kutiliwa shaka au ukiukaji wa masharti na sera zetu; na
 • vinginevyo kama ilivyoelekezwa au kuidhinishwa nawe.
Tunaweza pia kushiriki maelezo tunayokusanya na washirika wetu na wateja wanaotusaidia kutoa na kuboresha Huduma zetu au Huduma nyingine za Facebook au wanaotumia matangazo yetu au bidhaa kama hizo, hali inayotuwezesha kutoa Workplace Standard kama huduma bila malipo kwako. Hatutashiriki maelezo yanayokutambulisha kibinafsi (maelezo ya kumtambua mtu binafsi ni maelezo kama vile jina au anwani ya barua pepe ambayo inaweza kutumika pekee kuwasiliana nawe au kukutambulisha wewe) kwa washirika wa kuweka matangazo, upimaji au takwimu isipokuwa unapotupatia kibali. Tunaweza kutoa washirika hawa kwa maelezo kuhusu ufikiaji na ufanisi wa kutangaza bila kutoa maelezo ambayo hukutambua kibinafsi, au iwapo tumejumlisha maelezo ili yasikutambue kibinafsi.
Maombi ya kisheria. Tunaweza kufikia, kulinda na kushiriki majibu ya maelezo yako kwa maombi ya kisheria (kama udhamini wa utafutaji, agizo la mahakama au hati ya kuitwa mahakamani) iwapo tuna imani nzuri ambayo sheria hutuhitaji kufanya hivyo. Hii inaweza kuwa pamoja na kujibu maombi ya kisheria tunapoamini kuwa jibu hili linahitajika kisheria katika eneo hilo, linaathiri watumiaji walio katika eneo hilo na kwamba linazingatia vigezo vinavyotambulika kimataifa. Pia tunaweza kufikia, kuhifadhi na kushiriki maelezo tunapoamini kuwa ni muhimu: kutambua, kuzuia na kuzungumzia udanganyifu na shughuli nyingine za haramu; kujilinda, kukulinda wewe pamoja na wengine, pamoja na sehemu ya uchunguzi, au kuzuia kifo au madhara ya kimwili yanayokaribia kufanyika. Kwa mfano, tunaweza kutoa maelezo kwa washirika kuhusu uaminifu wa akaunti yako ili kuzuia ulaghai na matumizi mabaya ndani na nje ya Huduma zetu na Huduma nyingine ya Facebook. Maelezo tunayopokea kukuhusu yanaweza kufikiwa, kuchakatwa na kuhifadhi kwa muda mrefu ikiwa maelezo haya yanahitajika kwa wajibu au ombi la kisheria, uchunguzi wa kiserikali au uchunguzi dhidi ya uwezekano wa kuwepo kwa ukiukaji wa masharti na sera zetu au vinginevyo kuzuia madhara. Pia tunaweza kuhifadhi maelezo kutoka kwenye akaunti zilizolemazwa kwa ukiukaji wa masharti yetu kwa angalau mwaka mmoja ili kuzuia marudio ya matumizi mabaya au ukiukaji mwingine wa masharti yetu.
Data Jumlishwa au iliyoacha kutambulishwa. Tunaweza pia kutoa maelezo ambayo yamejumlishwa au ambayo vinginevyo hayakutambulishi kibinafsi kwa kampuni nyingine na washirika ambao wanaweza, pamoja na madhumuni mengine, kuyatumia kwa ajili ya uchanganuzi, kufuatilia mambo yanayovuma na uchanganuzi ili kuboresha na kutoa bidhaa na huduma zetu pamoja na bidhaa na huduma zinazotolewa na Kampuni za Facebook.

IV. Msingi wetu kuu wa kisheria wa kuchakata data ni upi?
Tunakusanya, kutumia na kushiriki data tuliyo nayo kwa njia zilizoelezwa hapo juu:
 • inavyohitajika kutimiza Masharti yetu ya Huduma;
 • inavyohitajika kuzingatia wajibu wetu kisheria; na
 • inavyohitajika kwa ajili ya matakwa yetu (au ya wengine), ikiwa ni pamoja na matakwa yetu ya kutoa huduma bunifu, ilibinafsishwa, salama na yenye manufaa kwa watumiaji na washirika, isipokuwa endapo matakwa yako yanapopiku matakwa yetu au haki za kimsingi na uhuru unaohitajika kulindwa kwa data ya kibinafsi.

V. Unaweza kutekeleza vipi haki zako zilizo katika mwongozo wa GDPR?
CChini ya Mwongozo wa Kanuni ya Kijumla ya Ulindaji wa Data, una haki ya kufikia, kurekebisha na kufuta data yako, pamoja na haki ya kuwekea vikwazo na kukataa uchakataji fulani wa data yako. Haya ni pamoja na:
 • pale ambapo umekubali uwekaji matangazo moja kwa moja, una haki ya kukataa uchakataji wetu wa data yako kwa madhumuni hayo, ni haki unayoweza kutekeleza kwa kutumia kiungo cha “jiondoe” katika mawasiliano ya matangazo kama hayo; na
 • haki ya kukataa uchakataji wetu wa data yako pale ambapo tunafuata matakwa yetu halali au yale ya mshirika ambayo unaweza kutekeleza kwa kutuomba kufuta akaunti yako wakati wowote.

VI. Uhifadhi wa Data, kufungwa na kufutwa kwa akaunti
Tunahifadhi data hadi pale ambapo hatuihitaji tena ili kutoa Huduma zetu au hadi pale akaunti yako inapofutwa- ile hali itakayotokea kwanza. Hii ni tathmini ya kila tukio inayotegemea mambo kama vile aina ya data, sababu ya kukusanywa na kuchakatwa kwake, mahitaji muhimu ya kisheria na kiutendakazi ya kuhifadhi data.
Unaweza kufuta akaunti yako wakati wowote. Unapofuta akaunti yako, tunafuta machapisho yako. Ikiwa hutaki kufuta akaunti yako, lakini unataka kuacha kutumia Workplace Standard kwa muda, tunaweza kukupa chaguo la kuzima akaunti yako badala yake. Ili upate maelezo zaidi kuhusu kufuta akaunti yako, bofya hapa na ili upate maelezo zaidi kuhusu kufunga akaunti yako, bofya hapa. Inaweza kuchukua hadi siku 90 kufuta data zilizohifadhiwa kwenye mfumo wako wa uhifadhi rudufu. Katika kipindi hiki, maelezo yako hayawezi kufikiwa kwenye Workplace.

VII. Je, unawezaje kufikia na kubadilisha maelezo tuliyo nayo yanayokuhusu?
Unaweza kupata zana za kudhibiti, kufikia na kuhamisha data yako Mipangilio ya Jumla ya Akaunti yako ya Workplace.
Unafikia, kurekebisha na kufuta maelezo ambayo umepakia kwenye Huduma kwa kutumia zana zilizo ndani ya Huduma inayotolewa nasi (kwa mfano, kubadilisha maelezo ya wasifu wako, kupitia kwenye Kumbukumbu ya Shughuli au kupakia na kuhamisha maelezo yako kupitia zana ya Pakua Maelezo Yako inayoweza kufikiwa kwenye Mipangilio ya Akaunti yako) Mabadiliko unayoyafanya kwenye maelezo yako kwenye Huduma yanaanza kutumika mara moja kwenye jumuiya yako lakini data itahifadhiwa na Facebook kwenye nakala rudufu kwa kipindi kifaacho kibiashara.

VIII. Usalama na Ulinzi
Tunatumia maelezo tuliyo nayo ili kusaidia kuthibitisha akaunti na shughuli na kuendeleza usalama kwenye na nje ya Huduma zetu, kama vile kwa kuchunguza shughuli za kutiliwa shaka au ukiukaji wa masharti na sera zetu. Tunafanya bidii ili kulinda akaunti yako kwa kutumia timu za wahandisi, mifumo ya kiotomatiki na teknolojia ya juu kama vile usimbaji kwa njia fiche na mafunzo ya kimashine. Kwa mfano, tunaweza kutumia teknolojia ya kiotomatiki kugundua tabia za matumizi mabaya na maudhui yasiyofaa kama vile ponografia ya watoto, yanayoweza kuathiri Huduma, wewe, watumiaji wengine na wengine. Baadhi ya vipengele vya Huduma vinaweza kuwa na viungo kwenye maudhui yanayohifadhiwa na washirika ambao sisi hatuwadhibiti. Hatuwajibikii matendo ya faragha ya washirika hawa na tunapendekeza kwamba uangalie sera za faragha ya kila tovuti unayotembelea.

IX. Jinsi huduma za kiulimwengu kufanya kazi
Katika kutoa Huduma kwako na katika kutumia watoa huduma waliorejelewa kwenye Sera hii ya Faragha, unaelewa kwamba maelezo yanaweza kuhifadhiwa au kuchakatwa nasi katika maeneo mbalimbali kote ulimwenguni. Kwa mfano, maelezo yaliyokusanywa katika Eneo la Kiuchumi la Ulaya (“EEA”) yanaweza kuhamishwa kwenye nchi zilizo nje ya EEA kwa madhumuni yaliyoelezwa kwenye sera hii. Tunatumia vifungu vya kawaida vya kandarasi ya kawaida vilivyoidhinishwa na Umoja wa Ulaya na kutegemea maamuzi toshelevu ya Umoja wa Ulaya kuhusu baadhi ya mataifa, inavyotumika kwa uhamishaji wa data kutoka Eneo la kiuchumi la Ulaya EEA hadi Marekani na nchi nyingine.

X. Je, tutakuarifu vipi kuhusu mabadiliko kwenye sera hii?
Tunaweza kusasisha Sera hii ya Faragha mara kwa mara. Tunaposasisha Sera ya Faragha, tutatoa taarifa ifaayo kwako, kubadilisha “Tarehe ya kuanza kutumika” iliyo hapo juu na tuchapishe Sera mpya ya Faragha.

XI. Jinsi ya kuwasiliana na Facebook ukiwa na maswali
Ikiwa una maswali yoyote kuhusu Sera hii ya Faragha, au ungependa kupata maelezo zaidi kwa ujumla kuhusu Workplace, Tafadhali wasiliana nasi mtandaoni uchapishe kwenye:
Facebook, Inc.
1601 Willow Road
Menlo Park, CA 94025, Marekani (ikiwa unaishi nje ya Umoja wa Ulaya)
AU
Facebook Ireland Ltd.
4 Grand Canal Square
Grand Canal Harbour
Dublin 2 Ireland (ikiwa unaishi katika Umoja wa Ulaya).
Unaweza pia kuwasiliana na Afisa wa Ulinzi wa Data wa Facebook Ireland Ltd.
Facebook Ireland Ltd. Inadhibitiwa nchini Ayalandi na Tume ya Ulindaji Data ya nchini Ayalandi.

Ilisasishwa mwisho: Tarehe 2 Septemba 2019

Taarifa ya Faragha kwa Wakaazi wa California(Tarehe ya Marekebisho ya Mwisho: Julai 1, 2020)

Taarifa Hii ya Faragha ya California (“Taarifa”) ni ya wakaazi wa California na inatumika kama ya ziada kwa Sera ya Faragha ya Workplace Standard iliyo hapa juu. Inaeleza jinsi tunavyokusanya, kutumia na kushiriki Maelezo yako ya Kibinafsi na jinsi ya kutekeleza haki zako chini ya Sheria ya Faragha ya Mtumiaji ya California (“CCPA”).
Tunaposema “Maelezo ya Kibinafsi” katika Taarifa hii, tunamaanisha maelezo yanayotambua, yanahusiana na, yanafafanua, yaliyo na uwezekano wa kuhusishwa na au yaliyo na uwezekano wa kuhusishwa nawe moja kwa moja au kwa njia isiyo ya moja kwa moja. Maelezo ya Kibinafsi hayajumuishi maelezo ambayo yamejumlishwa au maelezo ambayo hayawezi kuhusishwa nawe.

Jinsi tunavyokusanya, kutumia na kushiriki Maelezo ya Kibinafsi
Ili kulipa Jukwaa la Workplace Standard (ambalo linajumuisha tovuti, programu au huduma husiani za mtandaoni za Workplace, ambazo tunaziita “Huduma”), ni lazima tuchakate maelezo kukuhusu, ikiwa ni pamoja na Maelezo ya Kibinafsi. Kulingana na vikwazo tulivyofafanua hapa juu katika Sera yetu ya Faragha ya Workplace Standard, tunaweza kushiriki Maelezo yako ya Kibinafsi kwa madhumuni ya biashara kwa vikwazo madhubuti kuhusu jinsi washirika wetu wanaweza kutumia na kufichua data tunayoitoa, kwa mwelekeo wako au kwa njia ambazo vinginevyo vinalingana na CCPA. Hatuuzi Maelezo yako ya Kibinafsi na hatutafanya hivyo kamwe.
Njia bora zaidi ya kujifunza zaidi kuhusu aina za maelezo tunayokusanya na jinsi tunavyoyatumia ni kukagua Sera Yetu ya Faragha ya Workplace Standard. Ufuatao ni muhtasari wa kategoria zinazohusiana na CCPA za Maelezo ya Kibinafsi tunayoweza kukusanya kukuhusu katika kipindi cha miezi 12 iliyopita, kwa kutegemea unavyotumia Huduma, pamoja na jinsi tunavyoyatumia na wale tunaoweza kuyashiriki nao

Kategoria ya Maelezo ya Kibinafsi tunayokusanya inaweza kujumuisha:Mifano ya jinsi Taarifa Binafsi inatumika ni pamoja na:Wahusika ambao tunaweza kushiriki nao kila kategoria ya Maelezo ya Kibinafsi ni pamoja na:
 • Vitambuzi;
 • Taarifa ya shughuli ya intaneti au mitandao ya elektroniki;
 • Maelezo yanayohusiana na eneo, ikiwa ni pamoja na eneo halisi la kifaa ikiwa utachagua kuturuhusu kuyakusanya;
 • Maelezo ya sauti au onyesho, ikiwa ni pamoja na picha ikiwa wewe au wengine watachagua kutoa maelezo hayo;
 • Maelezo ya kitaaluma au ya kazi, ikiwa utaachagua kuyatoa; na
 • Maelezo yaliyotolewa kwenye Maelezo mengine ya Kibinafsi kukuhusu, ambayo yanaweza kujumuisha mapendeleo yako na maelezo mengine yanayotumika kukupa matumizi yaliyobinafsisha kwa ajili yako.
 • Kutoa, kubinafsisha na kuboresha Huduma;
 • Kukutumia mawasiliano ya mauzo;
 • Kuhimiza usalama, uadilifu na ulinzi; na
 • Kuwasiliana nawe.
 • Jumuiya unayochagua kushiriki na kuwasiliana nayo kupitia Huduma;
 • Biashara inayochukua udhibiti wa jumuiya yake ya Workplace, ilivyofafanuliwa kwenye Masharti ya Huduma ya Workplace Standard;
 • Watu na akaunti ambazo wengine hushiriki au kushiriki tena nao maudhui kukuhusu;
 • Washirika, ikiwa ni pamoja na washirika wanaotumia huduma za takwimu, watangazaji, washirika wa upimaji, washirika wanaotoa bidhaa na huduma katika Huduma zetu, wauzaji na watoa huduma;
 • Programu za watu wengine, tovuti au huduma nyingine unazoweza kuunganishwa nazo kupitia Huduma;
 • Wamiliki wapya kukitokea mabadiliko katika umiliki au udhibiti wa Huduma wetu wote au sehemu yake au mali zao kubadilika;
 • Utekelezaji wa sheria au wahusika wengine wanaohusishwa na maombi ya kisheria; na

Ili kujifunza zaidi kuhusu jinsi tunavyochakata maelezo, ikiwa ni pamoja na aina nyingine ya Maelezo ya Kibinafsi tunayoyakusanya, rejelea Sera yetu ya Faragha ya Workplace Standard.

Vyanzo vya Maelezo ya Kibinafsi
Tunapokea Maelezo ya Kibinafsi kutoka kwenye maelezo ambayo wewe na wengine hutoa, kutoka kwenye kifaa/vifaa vyako na kutoka kwa washirika wetu. Kategoria ya vyanzo ambavyo tunakusanya au kupokea maelezo ya kibinafsi kutoka kwavyo ni pamoja na:
 • Wewe: Tunakusanya maudhui na maelezo mengine unayotoa wakati unapotumia Huduma zetu, ikiwa ni pamoja na unapojiandikisha kupata akaunti, kuunda au kusambaza, na kutuma ujumbe au kuwasiliana na wengine. Hii inaweza kujumuisha maelezo ya au kuhusu maudhi unaotoa, kama vile tarehe ambapo faili fulani iliundwa. Pia tunakusanya maelezo kuhusu jinsi unavyotumia Huduma zetu, kama vile aina za maudhui unayotazama au kuhusiana nayo au kasi na muda wa shughuli zako. Pia tunakusanya maelezo kuhusu watu na vikundi ulivyounganishwa kwavyo na jinsi unavyoingiliana nao kama vile watu unaowasiliana nao sana au vikundi unavyopenda kushiriki navyo.
 • Watu wengine: Pia tunaweza kupokea mawasiliano na maelezo ambayo watu wengine hutoa wanapotumia Huduma. Haya yanaweza kujumuisha maelezo kukuhusu, kama vile wakati wengine wanashiriki au kutoa maoni kwenye picha yako, kukutumia au kupakia, kusawazisha au kuleta maelezo yako ya mwasiliani.
 • Kifaa/vifaa vyako: Tunaweza kukusanya maelezo kutoka au kuhusu kompyuta, simu au vifaa vingine ambapo umesakinisha au kufikia Huduma zetu. Tunaweza kuhusisha au kuunganisha maelezo tunayokusanya kutoka kwenye vifaa vyako tofauti yanayotusaidia kukupa Huduma thabiti kwenye vifaa vyako mbalimbali.
 • Kampuni za Facebook: Tunaweza kupokea maelezo kutoka Kampuni nyingine za Facebook (ambazo ni pamoja na WhatsApp na Oculus) kwa madhumuni ya biashara zinazotusaidia kukupa matumizi bunifu, muhimu, thabiti na salama katika Bidhaa Zote Mbalimbali za Kampuni ya Facebook unazotumia. Pia tunachakata maelezo kukuhusu kote kwenye Kampuni za Facebook kwa madhumuni haya, ilivyoruhusiwa na sheria inayotumika na kwa mujibu wa masharti na sera zao.
 • Washiriki: Pia tumaweza kupokea maelezo kutoka kwa washirika wetu kukuhusu na shughuli zako kwenye na nje ya Workplace, kama vile maelezo kutoka kwa mshirika tunapotoa huduma kwako kwa pamoja.

Je, unawezaje kutekeleza haki zako zilizotolewa chini ya CCPA?
Chini ya CCPA, una haki zifuatazo:
 • Haki ya Kufahamu: Una haki ya kuomba kwamba tukufichulie Maelezo ya Kibinafsi tunayokusanya, kutumia au kufichua na maelezo kuhusu matendo yetu ya data;
 • Haki ya Kuomba Data Yafutwe: Una haki ya kuomba kwamba tufute Maelezo yako ya Kibinafsi tunayokusanya kutoka kwako;
 • Haki ya Kutobaguliwa: Hatutakubagua kwa kutekeleza haki yoyote kati ya hizi.
Ili kutekeleza “haki ya kufahamu” au “haki yako ya kuomba yafutwe,” bofya hapa.
Tafadhali kumbuka kwamba tunalinda maelezo yako na uadilifu wa Huduma zetu, tunaweza kuhitaji kuthibitisha utambulisho wako kabla ya kuchakata ombi lako. Katika hali fulani, tunaweza kuhitaji kukusanya taarifa ya ziada ili kuthibitisha utambulisho wako kama vile Kitambulisho chako kilichotolewa na serikali.
Chini ya CCPA, unaweza kutekeleza haki hizi binafsi au unaweza kuteua ajenti aliyeidhinishwa kufanya maombi haya kwa niaba yako. Katika hali nyingi, tutawezesha ombi lako kwa kufanya zana za kiotomatiki kupatikana kupitia akaunti iliyolindwa kwa nenosiri

Anwani kwa ajili ya maelezo zaidi.
Ikiwa una maswali ya ziada kuhusu Taarifa hii au jinsi ya kutekeleza haki zako chini ya CCPA, tafadhali wasiliana nasi.