Sera Zinazokubalika za Matumizi ya Workplace


Karibu kwenye huduma ya Workplace kutoka Meta!
Tafadhali kumbuka kwamba hii ni huduma tofauti na toleo la mtumiaji la Facebook na inalenga kutumika na mashirika. Hii inamaanisha kwamba ikiwa unatumia huduma yetu kwenye workplace au kwenye kifaa au akaunti uliyopewa na mwajiri wako au shirika jingine (“Shirika” lako), Shirika hilo huenda lina sera zake binafsi zinazohusiana na matumizi yako ya Workplace na matumizi yako ya huduma yanafaa kuzingatia sera hizi. Tafadhali wasiliana a Shirika ikiwa una maswali kuhusiana na sera zake. Kwa maelezo kuhusu matendo ya faragha ya Workplace, tafadhali tembelea Sera ya Faragha ya Workplace. Fikia API za Workplace APIs zinazosimamiwa na Masharti ya Jukwaa la Workplace.

Kuwajibikia Matumizi ya Workplace
Pamoja na sera za Shirika lako, pia tumeunda kanuni zifuatazo ili kusaidia kuhakikisha unatumia huduma zetu kwa uwajibikaji.
Unapotumia Workplace, haupaswi kufanya yafuatayo:
  • Kuficha utambulisho wako, kutumia maelezo ya utambulisho ya mtu mwingine au kuwakilisha ushirika wako na mtu au shirika lolote bila idhini.
  • Kujihusisha katika shughuli yoyote inayotumia vibaya, kudhuru au kutishia kudhuru watoto.
  • Kuunda au kuonyesha maudhui yaliyopigwa marufuku, ya kubagua, yenye madhara, ya kilaghai, ya kudanganya au ya matusi, au yale yanayoendeleza au kuhimiza machafuko, ukiukaji wa sheria, uharibifu-binafsi, matatizo ya ulaji au matumizi mabaya ya dawa.
  • Kukiuka sheria au kuingilia haki za Meta au za mhusika mwingine.
  • Kuingilia utendakazi wa kawaida wa Workplace au kuingilia matumizi ya Workplace kwa mtu mwingine.
  • Kufikia Workplace au maudhui yanayohusiana nayo au maelezo kupitia njia ambazo hazijaidhinishwa na Meta (ikiwemo kupitia njia za kuvizia na kufumania); kubadilisha vidhibiti ufikiaji; au vinginevyo kujaribu kufikia Workplace na mifumo sawia, nenosiri au akaunti bila idhini.
  • Kushiriki maelezo ya kufikia msimamizi na au kutoa idhini kwa programu sawia kwa mtu yeyote yule ambaye hajaidhinishwa na Meta. Unapoamua kutoa idhini kama hiyo ya kufikia, ama kupitia maelezo au idhini kwa programu kwa mshirika ambaye ameidhinishwa, unaweza kumpa mshirika huyo idhini ya kufikia data yako au maudhui kadri tu data hiyo ikitumika kwa madhumuni yaliyoidhinishwa na Meta na kuambatana na maelezo yako. Tunasalia na haki ya kuwekea vikwazo ufikiaji kama huo wa washirika wengine (m.f kwa kuwekea mipangilio mipya maelezo ya ufikiaji au kuondoa ruhusa kwa programu) wakati wowote ikiwa tunaamini kuwa ufikiaji kama huo utatumika au umetumika vibaya.
  • Kupakia virusi, au misimbo mingine ya kuhadaa, au kufanya chochote kinachoweza kuharibu, kulemaza, kutwika mambo mengi au kutatiza utendakazi wa Workplace au mifumo sawia (kama vile mashambulizi ya kukataza huduma au kuingillia utoaji wa ukurasa au vipengele vingine vya Workplace).
Tafadhali pia kumbuka kwamba Workplace haifai kutumiwa na watoto wenye umri wa chini ya miaka 13, kwa hivyo ikiwa una umri wa chini ya miaka 13, huruhusiwi kufikia au kutumia huduma hii.

Wajibu wetu na maoni yako
Meta inaweza kutumia teknolojia ya kiotomatiki kugundua ponografia ya watoto, maudhui mengine yaliyopigwa marufuku au maudhui yoyote ambayo tunaamini kwamba yanaweza kudhuru Workplace, watumiaji na wahusika wengine.
Tunaweza (lakini hatuna wajibu huo wa) kuondoa au kuwekea vikwazo ufikiaji wa data au maudhui yoyote ikiwa tunaamini kwamba yanakiuka Sera Inayokubalika ya Matumizi, Mkataba wa Shirika lako wa Wateja wa Workplace au sheria na masharti husika. Meta itakupa au Shirika lako ilani ifaayo ya hatua kama hiyo isipokuwa ikiwa imepigwa marufuku kisheria.
Tunakaribisha maoni yote kuhusu Workplace, lakini kumbuka kwamba tutatumia maoni au mapendekezo yako bila wajibu wowote au fidia kwako.

Ilisasishwa mwisho: 10 Januari 2022