Sera ya Vidakuzi vya Tovuti ya Workplace


Sera hii ya Vidakuzi vya Tovuti ya Workplace (“Sera ya Vidakuzi vya Tovuti”) inafafanua jinsi tunavyotumia vidakuzi kwenye Tovuti ya Workplace (kama ilivyofafanuliwa hapa chini) na inapaswa kusomwa pamoja na Sera ya Faragha ya Mauzo ya Workplace ambayo itatumika kuchakata data yetu ya kibinafsi tunayokusanya kupitia vidakuzi. Sera hii ya Vidakuzi vya Tovuti haitumiki kwa matumizi yako ya bidhaa ya mtandaoni ya Workplace ambayo tunawapa wateja wetu (shirika unalolifanya kazi), inayoruhusu watumiaji kushirikiana na kushiriki maelezo kazini, ikiwemo bidhaa ya Workplace, programu na huduma zinazohusiana za mtandaoni (pamoja “Huduma za Workplace”). Kwa maelezo kuhusu jinsi tunavyotumia vidakuzi kwenye Huduma za Workplace, tafadhali tazama Sera ya Vidakuzi vya Workplace.
Vidakuzi na Teknolojia Nyingine za Hifadhi
Vidakuzi ni matini madogo yanayotumiwa kuhifadhi maelezo kwenye vivinjari vya wavuti. Vidakuzi vinatumiwa kuhifadhi na kupokea vitambulishi na maelezo mengine kwenye kompyuta, simu, na vifaa vingine. Teknolojia zingine, pamoja na data tunayohifadhi kwenye kivinjari chako cha wavuti au kifaa, vitambuzi vinavyohusiana na kifaa chako, na programu nyingine, hutumiwa kwa malengo sawa. Katika sera hii, tunarejelea teknolojia hizi zote kama “vidakuzi”.
Tunatumia vidakuzi wapi?
Tunaweza kuweka vidakuzi kwenye kompyuta au kifaa chako, na kupokea maelezo yaliyohifadhiwa kwenye vidakuzi, unapotembelea tovuti yetu ya mauzo ya umma na taarifa, Workplace.com (“Tovuti ya Workplace”)
Vidakuzi hudumu kwa muda gani?
Vidakuzi vyote vina tarehe za mwisho wa matumizi ambazo hubainisha muda wa kukaa kwenye kivinjari chako au kwenye kifaa chako na hivi vinaweza kugawanywa katika vikundi viwili:
  • Vidakuzi vya Kipindi – hivi ni vidakuzi vya muda ambavyo huisha muda wake (na hufutwa kiotomatiki) kila wakati unapofunga kivinjari chako.
  • Vidakuzi vya Kujirudia – kwa kawaida huwa na tarehe ya mwisho wa matumizi na kwa hivyo hubaki kwenye kivinjari chako hadi muda wake wa matumizi kuisha, au hadi uvifute wewe mwenyewe.
Kwa nini tunatumia vidakuzi?
Vidakuzi hutusaidia kutoa, kulinda na kuboresha Tovuti yetu ya Workplace, kama vile kubinafsisha maudhui na kutoa uzoefu salama.
Hasa, tunazitumia kwa madhumuni yafuatayo:
Aina ya KidakuziLengo
Usalama, tovuti na uadilifu wa bidhaa
Tunatumia vidakuzi ili kutusaidia kuweka Tovuti ya Workplace kuwa salama na iliyolindwa.
Pia tunatumia vidakuzi kupambana na shughuli zinazokiuka sera zetu au vinginevyo zinashusha hadhi ya uwezo wetu wa kutoa Tovuti ya Workplace.
Vipengele na huduma za tovuti
Tunatumia vidakuzi kutoa vipengele vinavyotusaidia kukupa Tovuti ya Workplace.
Kwa mfano: Vidakuzi hutusaidia kuhifadhi mapendeleo, kujua unapoona au kutagusana na maudhui ya Workplace, na kukutolea maudhui na tajiriba zilizogeuzwa kukufaa.
Pia tunatumia vidakuzi ili kusaidia kukutolea maudhui muhimu kwa eneo lako.
Kwa mfano: Tunahifadhi maelezo kwenye kidakuzi kinachowekwa kwenye kivinjari au kifaa chako ili uweze kuona Tovuti ya Workplace katika lugha yako unayopendelea.
Utendaji
Tunatumia vidakuzi ili kukutolea hali nzuri ya matumizi iwezekanavyo.
Kwa mfano: Vidakuzi hutusaidia kupanga trafiki kati ya seva na kuelewa Tovuti ya Workplace hupakiwa haraka kiasi gani kwa watu tofauti. Vidakuzi pia hutusaidia kurekodi vipimo na ukubwa wa skrini na madirisha yako na kujua ikiwa umewasha hali ya juu ya ubainifu ili tuweze kuwasilisha Tovuti yetu ipasavyo.
Uchanganuzi na utafiti
Tunatumia vidakuzi ili kuelewa vyema jinsi watu hutumia Tovuti ya Workplace ili tuweze kuiimarisha.
Kwa mfano: Vidakuzi vinaweza kusaidia kuelewa jinsi watu hutumia Tovuti ya Workplace, kuchanganua sehemu zipi za Tovuti ya Workplace ambazo zinawafaidi sana watu na kuhusisha na kutambua vipengele vinavyoweza kuboreshwa.
Utangazaji na upimaji
Tunatumia vidakuzi kwenye Tovuti ya Workplace, ikiwemo Facebook pixel na vidakuzi vya wahusika wengine na lebo zilizofafanuliwa, ili kutusaidia kutangaza Workplace kwa watu ambao wanaweza kupendezwa na Huduma za Workplace. Hatuweki vidakuzi hivi kwenye Huduma za Workplace.
Kwa mfano: Vidakuzi hutuwezesha kusaidia kulenga matangazo kwa watu ambao awali walitembelea Tovuti ya Workplace.
Pia tunatumia vidakuzi kusaidia kupima utendaji wa kampeni zetu za matangazo na kuelewa ikiwa unashirikiana na mawasiliano yetu.

Tunatumia vidakuzi gani?
Vidakuzi ambavyo tunamia vinajumuisha vidakuzi vya kipindi, vinavyofutwa unapofunga kivinjari chako, na vidakuzi vya kila mara, vinavyokaa kwenye kivinjari chako hadi viishe muda au uvifute.
Tunatumia vidakuzi vya wahusika wa kwanza na wahusika wengine. Vidakuzi vya mhusika wa kwanza ni vidakuzi ambavyo tumeweka ili kukusanya maelezo kukuhusu. Vidakuzi vya wahusika wengine huwekwa na wahusika wengine ambao wanatupa huduma. Hii inamaanisha kwamba maelezo kukuhusu ambayo yanakusanywa na vidakuzi hivyo vya wahusika wengine yatashirikiwa na wahusika wengine wanaofaa na yanaweza kutumiwa na wahusika wengine kwa mujibu wa ilani yao ya faragha.
Vidakuzi na lebo za wahusika wengine
Iwapo umechagua kuruhusu vidakuzi na lebo za wahusika wengine, pia tunaweka vidakuzi vinavyofanya kazi na huduma ya Uchanganuzi wa Google na huduma zingine za wahusika wengine zilizotajwa hapa chini kwenye Tovuti yetu ya Workplace ili kutusaidia kuelewa jinsi watumiaji hutumia Workplace, kuonyesha matangazo na kuelewa utendakazi wa matangazo yetu. Kwa sasa tunatumia vidakuzi vya wahusika wengine vifuatavyo:

Unawezaje kudhibiti matumizi yetu ya vidakuzi
Kivinjari au kifaa chako kinaweza kutoa mipangilio inayokuruhusu kuchagua iwapo vidakuzi vya kivinjari vimewekwa na kuvifuta. Kwa maelezo zaidi kuhusu vidhibiti hivi, tembelea nyenzo za msaada za kivinjari au kifaa chako.
Mipangilio ya kivinjari chako inaweza kukuruhusu kutuma ishara ya “Usifuatilie” unapotembelea tovuti mbalimbali. Kama tu tovuti nyingi, tovuti yetu haijaundwa kujibu ishara za “Usifuatilie” zinazopokewa kutoka kwa vivinjari. Ili kujifunza zaidi kuhusu ishara za “Usifuatilie”, unaweza kutembelea http://www.allaboutdnt.com/.

Zaidi ya hayo, ikiwa hutaki vidakuzi kudondoshwa na Google Analytics, unaweza kusakinisha programu jalizi ya kivinjari ya kujiondoa kwenye Google Analytics, ambayo hufanya kazi kwenye baadhi ya vivinjari pekee. Kwa maelezo zaidi kuhusu Takwimu za Google na matumizi yake ya vidakuzi, tafadhali tembelea “Jinsi Google hutumia data unapotumia tovuti au programu za washirika wetu”.
Huenda sehemu fulani za Tovuti ya Workplace zikakosa kufanya kazi ipasavyo ikiwa umelemaza vidakuzi.

Tarehe ya marekebisho ya mwisho: Septemba 16, 2022