Kiamabatisho cha Uchakataji wa Data

 1. Ufafanuzi
  Katika Kiambatisho Hiki cha Uchakataji wa Data, “GDPR” inamaanisha Kanuni za Kijumla za Ulindaji wa Data (Regulation (EU) 2016/679), na “Mdhibiti”, “Mchakataji Data”, “Mmiliki wa Data”, “Data ya Kibinafsi”, “Ukiukaji wa Data” na “Uchakataji” yote yatakuwa na maana sawa kama ilivyofafanuliwa kwenye GDPR. “Imechakatwa” na “Chakata” yataeleweka kulingana na ufafanuzi kuhusu maana ya “Uchakataji”. Istilahi nyingine zote zilizofafanuliwa hapa zitakuwa na maana sawa kama zilivyofafanuliwa kwingineko kwenye Makubaliano haya.
 2. Uchakataji wa Data
  1. Kwa kutekeleza shughuli zake kama Mchakataji chini ya Makubaliano haya kuhusiana na Data yoyote ya Kibinafsi kwenye Data Yako (“Data Yako ya Kibinafsi”), Facebook inathibitisha kwamba:
   1. kipindi, mada, hali na madhumuni ya Uchakataji huu yatabainishwa kwenye Makubaliano haya;
   2. aina za Data ya Kibinafsi Zinazochakatwa zitajumuisha zile zilizobainishwa kwenye ufafanuzi wa Data Yako;
   3. kategoria za Wamiliki wa Data zinajumuisha wawakilishi wako, Watumiaji na watu wengine waliotambuliwa au wanaweza kutambulika kupitia Data Yako ya Kibinafsi; na
   4. majukumu na haki zako kama Mdhibiti Data kuhusiana na Data yako ya Kibinafsi zimeelezwa kwenye Makubaliano haya.
  2. Kwa kiwango ambacho Facebook Huchakata Data yako ya Kibinafsi chini ya au kuhusiana na Makubaliano, Facebook:
   1. itachakata tu Data yako ya Kibinafsi kulingana na maelezo yako kama yalivyoelezwa kwenye Makubaliano haya, ikiwa ni pamoja na kwa mujibu wa uhamishaji wa Data yako ya Kibinafsi, kwa kutegemea hali za kipekee zilizoruhusiwa chini ya Kifungu cha 28(3)(a) cha GDPR;
   2. itahakikisha kwamba wafanyakazi wake walio na idhini ya Kuchakata Data Yako ya Kibinafsi chini ya Makubaliano haya wameapa kuzingatia siri au wanadhibitiwa na sheria kuhusu majukumu ya kulinda siri kuhusiana na Data yako ya Kibinafsi;
   3. itatekeleza hatua za kiufundi na za kishirika zilizobainishwa kwenye Kiambatisho cha Usalama wa Data;
   4. itazingatia kanuni zinazorejelewa hapa chini kwenye Sehemu ya 2.c na 2.d ya Kiambatisho cha Uchakataji Data inapowateua Wachakataji- wa kiwango cha chini;
   5. itakusaidia kwa kukupa hatua zifaazo za kiufundi na za kishirika kadri hii inavyowezekana kupitia Workplace, ili kukuwezesha kutimiza wajibu wako wa kujibu maombi ya Mmiliki Data ya kutekeleza haki chini ya Sura ya III ya GDPR;
   6. itakusaidia kuhakikisha unazingatia majukumu yako kwa mujibu wa Kifungu cha 32 hadi 36 ya GDPR kwa kuzingatia hali ya Uchakataji na maelezo yanayotolewa kwa Facebook;
   7. endapo Mkataba utasitishwa, Facebook, itafuta Data ya Kibinafsi kwa mujibu wa Mkataba isipokuwa endapo Umoja wa Ulaya au sheria za nchi mwanachama zitahitaji kwamba Data ya Kibinafsi ihifadhiwe;
   8. itakupa maelezo yote yaliyoelezwa kwenye Makubaliano haya na kupitia Workplace katika kutimiza majukumu ya Facebook ya kutoa maelezo yote muhimu ili kuonyesha Facebook inazingatia majukumu yake chini ya Kifungu cha 28 cha GDPR; na
   9. baada ya kila mwaka, Facebook inakubali kwamba itachagua kampuni nyingine itakayoendesha shughuli ya ukaguzi ya SOC 2 Aina ya II au ukaguzi mwingine unaokubalika kitaaluma wa udhibiti wa Facebook kuhusiana na Workplace, unazipa uwezo kikazi kampuni nyingine kama hizo. Ikiwa utaomba, Facebook itakupa nakala ya ripoti ya ukaguzi ya wakati huo na ripoti kama hiyo itazingatiwa kuwa ni Maelezo ya Siri ya Facebook.
  3. Unaidhinisha Facebook kuwapa kandarasi ya majukumu ya Uchakataji data chini ya Makubaliano haya kwa Washirika wa Facebook, na kwa kampuni nyingine, orodha ambayo Facebook itakupa baada ya kupokea ombi lako kwenye andiko. Facebook itafanya hivyo tu kwa kuwepo makubaliano yaliyoandikwa kati yake na Wachakataji-wengine kama hao, makubaliano ambayo yanaweka majukumu sawa ya ulindaji wa data kwa Wachakataji-wengine kama yalivyowekwa kwa Facebook chini ya Makubaliano haya. Pale ambapo Mchakataji-mwingine huyo anaposhindwa kutimiza majukumu kama hayo, Facebook itakuwa na wajibu kikamilifu kwa utenmwa kukuhakikishia kwamba Mchakataji-mwingine anazingatia majukumu yake ya kulinda data.
  4. Pale ambapo Facebook inahusisha au kubadilisha Mchakataji-mwingine kuanzia (i) 25 Mei 2018, au (ii) Tarehe ya Kuanza kutumika (Tarehe yoyote ile itakuja baadaye), Facebook itakuarifu kuhusu kuongezwa huko au kubadilishwa kwa Wachakataji-wengine katika muda usiozidi siku kumi na nne (14) kabla ya kuteuliwa kwa au kubadilishwa kwa Mchakataji-mwingine kama huyo. Unaweza kukataa kuhusishwa kwa au kubadilishwa kwa Mchakataji-mwingine kama huyo katika muda wa siku kumi na nne (14) baada ya kuarifiwa na Facebook kwa kusitisha Makubaliano haya mara moja kwa ilani ya maandishi ya Facebook.
  5. Facebook itakuarifu bila kuchelewa baada ya kujulishwa kuhusu Ukiukaji wa Data ya Kibinafsi unaohusiana na Data Yako ya Kibinafsi. Ilani kama hiyo itajumuisha, wakati wa taarifa au pindi tu baada ya taarifa, maelezo muhimu ya Ukiukaji wa Data ya Kibinafsi wanapopokea arifa au haraka iwezekanavyo baada ya kupokea ilani ikiwemo idadi ya rekodi zako zilizoathirika, kategoria na idadi ya Watumiaji walioathirika, madhara yanayotarajiwa ya ukiukaji huo na suluhu halisi au pendekezwa, panapofaa za kukabili athari zozote mbaya zinazoweza kutokana na ukiukaji huo.