Sera ya Faragha ya Workplace


Workplace from Meta ni jukwaa la mtandaoni lililoundwa na Meta linaloruhusu watumiaji kushirikiana na kushiriki maelezo kazini. Jukwaa la Workplace hujumuisha tovuti, programu na huduma husika za mtandaoni za Workplace, kwa pamoja “Huduma”.
Sera hii ya Faragha inafafanua jinsi maelezo yako hukusanywa, kutumiwa na kushirikiwa unapotumia Huduma hii.
Huduma hii inalenga kutumiwa na mashirika na kulingana na maelekezo yao na inatolewa kwako na mwajiri wako au shirika jingine ambalo limekupa idhini ya kufikia na kutumia Huduma hii (Shirika” lako).
Huduma hii ni tofauti na huduma nyingine za Meta ambazo unaweza kutumia. Huduma hizo nyingine za Meta zinatolewa kwako na Meta na zinadhibitiwa na masharti yao binafsi. Hata hivyo, Huduma hii inatolewa na Shirika lako na inadhibitiwa na Sera hii ya Faragha na Sera ya Ukubalifu ya Matumizi ya Workplace na Sera Vidakuzi vya Workplace.
Shirika lako linawajibikia na husimamia akaunti yako ya Workplace (“Akaunti Yako”). Shirika lako pia linawajibikia ukusanyaji na matumizi ya data unayowasilisha au kutoa kupitia Huduma hii na matumizi kama hayo hudhibitiwa na masharti ambayo Shirika lako limeweka pamoja na Meta.
Pamoja na Taarifa hii ya Faragha, Shirika lako linaweza kuwa na sera za ziada au utaratibu wa kitabia ambao unaweza kutumika kuhusiana na matumizi yako ya Huduma hii.
Ikiwa una maswali yoyote kuhusu matumizi yako ya Huduma, tafadhali wasiliana na Shirika lako.

I. Ni aina gani ya maelezo hukusanywa?
Shirika lako litakusanya aina zifuatazo za maelezo wewe, wafanyakazi wenzako au watumiaji wengine wanapofikia Huduma:
 • Maelezo yako ya anwani kama vile majina kamili na anwani ya barua pepe;
 • Jina lako la matumizi na nenosiri;
 • Nafasi yako kazini, maelezo ya idara na maelezo mengine yanayohusiana na kazi au Shirika lako.
 • Maudhui, mawasiliao na maelezo mengine unayotoa unapotumia Huduma hii, ikiwemo unapojisajili kwa akaunti, kuunda au kushiriki maudhui na kuwatumia ujumbe au kuwasiliana na watu wengine. Haya yanaweza kujumuisha maelezo ya au kuhusu maudhui unayotoa (kama vile metadata), kama vile mahali picha ipo au tarehe ambapo faili iliundwa;
 • Maudhui, mawasiliano na maelezo ambayo watu wengine hutoa wanapotumia Huduma hii. Hii inaweza kuwa pamoja na maelezo kukuhusu, kama vile wanaposhiriki au kutoa maoni kwenye picha yako, wanapokutumia ujumbe, wanapopakia, sawazisha au kuhamisha maelezo yako ya anwani;
 • mawasiliano yote na watumiaji wengine wa Huduma;
 • mawasiliano yote ya watumiaji, maoni, mapendekezo na mawazo yaliyotumwa kwenye Shirika lako;
 • maelezo ya bili; na
 • maelezo ambayo unatoa wakati wewe au Shirika lako linawasiliana au kuwasiliana na timu ya usaidizi ya jukwaa kuhusiana na Huduma hii.

II. Je, shirika lako hutumia taarifa hii kwa njia gani?
Shirika lako litashiriki na Meta maelezo litakayokusanya, kama mtoaji wa jukwaa ili kuruhusu Meta kutoa na kuendeleza Huduma kwa Shirika lako na watumiaji wengine na kwa kulingana maagizo mengine kutoka katika Shirika lako. Mifano ya hayo ni pamoja na:
 • Kuwasiliana na watumiaji na wasimamizi kuhusiana na matumizi yao ya Huduma;
 • Kuimarisha usalama wa Huduma kwa Shirika lako na watumiaji wengine kama vile kwa kuchunguza shughuli za kutiliwa shaka au ukiukaji wa masharti au sera zinazotumika;
 • kubinafsisha tajiriba yako pamoja na Shirika lako kama sehemu yetu ya utoaji wa Huduma;
 • kuunda zana, bidhaa au huduma mpya kwenye Huduma kwa ajili ya Shirika lako;
 • kuhusisha shughuli kwenye Huduma katika vifaa mbalimbali vinavyotumiwa na mtumiaji sawa kuboresha utendakazi wa jumla wa Huduma;
 • kutambua na kurekebisha hitilafu ambazo huenda zipo; na
 • kuendesha uchanganuzi wa data na mfumo, ikiwemo utafiti wa kuboresha Huduma.

III. Ufichuzi wa maelezo
Shirika lako litatoa maelezo yaliyokusanywa kwa njia zifuatazo:
 • kwa kampuni nyingine wanaotoa huduma ambayo husaidia katika kutoa Huduma au sehemu ya Huduma;
 • kwkwa programu, tovuti au huduma nyingine za kampuni nyingine ambazo unaweza kujiunganisha kwazo kupitia Huduma;
 • kuhusiana na mchakato muhimu wa kibiashara, kama vile uhamishaji wa Huduma, kuungana kwa kampuni, kuimarisha, uuzaji wa mali au katika tukio lisilotarajiwa la kufilisika au kutokuwa na pesa;
 • kulinda usalama wa mtu yeyote; kushughulikia ulaghai, usalama au hitilafu za kiufundi; na
 • kuhusiana na notisi, kibali, agizo la ugunduzi au ombi lolote au agizo kutoka katika shirika la kutekeleza sheria.

IV. Kufikia na kubadilisha maelezo yako
Wewe pamoja na Shirika lako mnaweza kufikia, kurekebisha au kufuta maelezo ambayo umepakia kwenye Huduma hii kwa kutumia zana zilizo kwenye Huduma (kwa mfano, kuhariri maelezo ya wasifu wako au kupitia Kumbukumbu ya Shughuli). Ikiwa umeshindwa kufanya hivyo kwa kutumia zana zilizotolewa kwenye Huduma, unafaa kuwasiliana na Shirika lako moja kwa moja au ukabadilishe maelezo yako.

V. Viungo na maudhui ya wahusika wengine
Huduma inaweza kuwa na viungo vya maudhui vinavyolindwa na wahusika wengine ambavyo havidhibitiwi na Shirika lako. Unafaa kukagua sera ya faragha ya kila tovuti unayotembelea.

VI. Kufungwa kwa Akaunti
Ikiwa ungependa kuacha kutumia Huduma hii, unafaa kuwasiliana na Shirika lako. Vilevile, ikiwa utaacha kufanyia kazi au kufanya kazi pamoja na Shirika, Shirika linaweza kusitisha matumizi ya Akaunti yako na/au kufuta maelezo yoyote yanayohusishwa na Akaunti Yako.
Kwa kawaida huchukua siku 90 kufuta akaunti baada ya kufunga kwake, lakini maelezo fulani huenda yakabaki katika nakala rudufu katika kipindi fulani halali. Tafadhali kumbuka kwamba maudhui unayounda na kushiriki kwenye Huduma hii humilikiwa na Shirika lako na huenda ikabaki kwenye Huduma na kufikiwa hata ikiwa Shirika lako litafunga au kusitisha Akaunti Yako. Katika hali hii, maudhui unayotoa kwenye Huduma hufanana na aina nyingine za maudhui (kama vile mawasilisho au memo) ambazo huenda ulizalisha wakati ukifanya kazi.

VII. Mabadiliko kwenye Sera ya Faragha
Sera hii ya Faragha huenda ikasasishwa mara kwa mara. Ikisasishwa tarehe “iliyosasishwa mwisho” hapo chini itarekebishwa na Sera mpya ya Faragha itachapishwa mtandaoni.

VIII. Mawasiliano
Ukiwa na maswali yoyote kuhusu Sera hii ya Faragha au Sera ya Ukubalifu ya Matumizi ya Workplace, tafadhali wasiliana na Shirika lako kupitia msimamizi wa Shirika lako.
Kwa wakaazi wa California, unaweza kujifunza zaidi kuhusu haki zako za faragha za mtumiaji kwa kuwasiliana na Shirika lako kupitia Msimamizi wa Shirika lako.

Ilisasishwa mwisho: 5 Aprili 2022